Friday 20 March 2015

Tanesco yatoa kauli kuhusu umeme kukatika mara kwa mara.........

Shirika la umeme nchni-Tanesco-limesema hakuna mgao wa umeme na kilichojitokeza kufuatia kukatika kwa umeme mara kwa mara kuanzia machi 15 ni uchakavu wa miundombinu ya umeme ikiwemo kuanguka kwa nguzo za umeme hususani katika maeneo ya makazi ya watu yasiyopimwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake kukosa umeme kwa wakati tofauti kuanzania machi 15 hadi 18 mwaka huu, meneja wa kanda wa Tanesco, mhandishi Mahenge Mugaya amesema changamoto kubwa inayoikabili Tanesco ni uchakavu wa nguzo na nyaya za kusafirisha umeme ambapo katika baadhi ya maeneo yasiyopimwa kumekuwa na tatizo la magari kugonga nguzo na umeme hali inayosababisha mitambo ya shirika hilo kukata umeme ili kuzuia madhara kwa jamii.
Aidha amesema shirika la umeme nchni limetenga bajeti ya shilingi bilioni 10 katika mpango wa miaka mitatu wa kuimarisha umeme katika jiji la Dar es Salaam, mpango utakaowezesha kuondoa nguzo mbovu, miti iliyokatika njia za umeme na kuimarisha vituo vidogo vya kusambaza umeme na kusisitiza shirika hilo limeshafanya tathimini ya nguzo mbaovu zote katika njia za umeme na kuandaa mpango kazi ili kuwa na mfumo mzuri wa usambazaji umeme.

0 comments:

Post a Comment