Tuesday, 17 March 2015

TAKUKURU Kuwaanika mtandaoni wala Rushwa..




Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imetangaza katika tovuti yake majina 287 ya washtakiwa waliopatikana na hatia katika kesi za rushwa.

Miongoni mwa majina yaliyotangazwa kupitia tovuti yake www.pccb.go.tz wamo wafanyabiashara, wanasiasa, waandishi wa habari, walimu, wauguzi, polisi, mwanafunzi na watumishi mbalimbali wa umma.
Hatua hiyo ya Takukuru ni mwanzo wa mfumo na utaratibu mpya ulioanzishwa na taasisi hiyo wa kuwatangaza hadharani washtakiwa wote waliopatikana na hatia katika kesi zinazohusu rushwa.
Ofisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Doreen Kapwani alisema jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa, utaratibu huo ambao umeanza kutumika Machi mwaka huu ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Mkurugenzi wa TAKUKURU Dr. Edward Hosea,amesema watu watakaokutwa na hatia kwa kuhusika na rushwa watatangazwa hadharani, ikiwa ni mkakati mpya ulionzishwa na Serikali kuonyesha ni jinsi gani inachukua hatua dhidi ya mapambano ya rushwa, ambapo majina hayo yatawekwa katika mtandao wa PCCB.


Msikie hapa chini Mkurugenzi wa TAKUKURU Dr. Edward Hosea akieleza juu ya uamuzi huo.







                                                                                            

0 comments:

Post a Comment