Saturday, 21 March 2015

Issue nzima ya Zitto kujiuzulu Ubunge.

 
Jana Kikao cha Bunge kilikuwa kikiendelea Dodoma, Mbunge Zitto Kabwe alikuwa mmoja ya Wabunge waliochangia katika mjadala uliokuwa unaendelea jioni ya jana kabla ya kupewa nafasi ya kusimama na kutoa maelezo binafsi.

Mwenyekiti wa Bunge Mussa Zungu alimpa nafasi hiyo Zitto Kabwe ambaye alisimama na kuanza kuongea; “Nashukuru kwa kunipa fursa hii kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge wenzangu.. 
Leo mchana nimemuandikia barua Mheshimiwa Spika ya kung’atuka Ubunge sina sababu ya kwenda kwenye details kuhusiana na jambo hilo kwa sababu taarifa ambayo nilikuwa nimeandaa kuitoa jana imesambaa na ipo na nitaisoma kwenye vyombo mbalimbali vya habari…“
Mnamo tarehe 10 March 2015 Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA akiwa makao makuu ya Chama hicho akiambatana na Katibu Mkuu wa CHADEMA alitangaza kuwa Chama hicho kimenifukuza uanachama…Nimeamua kutii uamuzi wa CHADEMA na hivyo kung’atuka rasmi…
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwenu Wabunge wote kwa yale yote ambayo tumeyafanya pamoja kwa ajili ya nchi yetu. Tumefurahi pamoja.. 
Tumehuzunika.. Tumelia.. Tumeisimamia pamoja Serikali na ninajivunia kuwa sehemu ya Bunge hili la kumi.. Na Mungu akipenda tutakuwa pamoja mwezi November… Kwaherini.. Asanteni sana”



Related Posts:

  • MSOMI AVUA NGUO KWA KUFUNGIWA OFISI… Hatua ya mwanamke mmoja msomi ya kuvua nguo nchini Uganda, imezua mjadala mkali nchini humo. Baada ya kukerwa na hatua ya kufungiwa nje ya ofisi yake na usimamizi wa chuo kikuu cha Makerere, Stella Nyanzi alivua nguo zo… Read More
  • MALKIA ELIZABETH ATIMIZA MIAKA 90… Siku ya leo tarehe 21-4-2016 Malkia Elizabeth ametimiza miaka tisini ya kuzaliwa. Malkia atasheherekea siku hii kwa kukutana na wananchi wake katika matembezi atayafanya huko Windsor. Malkia Elizabeth ametawala kwa mu… Read More
  • CANADA KUHALALISHA MATUMIZI YA BANGI..!! Serikali ya Canada itabuni sheria mpya mwaka ujao, ambazo zitahalalisha uuzaji wa bangi. Iwapo sheria hiyo itaidhinishwa italiorodhesha taifa la Canada, miongoni mwa mataifa yenye uchumi mkubwa magharibi kukubali matumi… Read More
  • MWANAMKE MTUMWA KUWEKWA KWENYE DOLA MAREKANI… Picha ya mtumwa mmoja aliyekata nyororo na kisha kusaidia mamia ya wenzake kutoroka utumwa, sasa itatumika katika noti mpya ya dola 20 nchini Marekani. Bi Harriet Tubman atakuwa Mwafrika Mmarekani wa kwanza, kuingizwa k… Read More
  • WANANE MBARONI KWA KUNYWA POMBE MCHANA… Wilaya ya Sengerema imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais, baada ya kukamata watu wanane waliokutwa wakinywa pombe saa za kazi. Amri ya kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa watu hao ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilay… Read More

0 comments:

Post a Comment