Matukio ya ukatili dhidi ya albino yanaendelea kuwa tishio nchini,baada ya mtoto wa miaka sita kukatwa kiganja cha mkono Shambulio hilo jipya limetokea mkoani Rukwa kusini magharibi mwa nchi hiyo, ambapo usiku wa kuamkia jana watu wasiojulikana walimshambulia na kumkata kiganja mtoto mwenye umri wa miaka sita, Baraka Cosmas na kisha kutokomea nacho kusikojulikana. Tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Kipeta Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga,ambako mtoto huyo anaishi na wazazi wake, Cosmas Yoram (32) na Prisca Shaaban. Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Jacob Mwaruanda,amesema tukio hilo ni la saa 8 usiku wa kuamkia Jumapili wakati mtoto huyo akiwa amelala na mama yake huku Baba wa mtoto huyo hakuwepo wakati huo. Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi la Under The Same Sun Vicky Mketema,amezungumzia jinsi ukatili huo unavyofanyika. Na kwanza ameanza kwa kuzungumzia kwa uapnde wa watu ambao wanataka kupata madini,kuwa wanaamini kuwa mguu wa albino unaweza kuwa msaada kwao kufanikiwa katika hilo,msikie hapa chini. https://soundcloud.com/wilberd-kiwale/wanga-wasema-viungo-vya-albino-vinavyotumika
TOTALERNEGIES MARKETING TANZANIA LTD KUPITIA MFUKO WA ELIMU WA TAIFA YATOA
KATONI 360 ZA TAULO ZA KIKE KWA SHULE NNE ZA SEKONDARI.
-
Dodoma
Kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd leo tarehe 22 Novemba 2024
imekabidhi katoni 360 za taulo za kike zenye thamani ya takribani Sh.
M...
2 hours ago
0 comments:
Post a Comment