Friday, 20 March 2015

Mauwaji ya Albino ni Janga la Taifa Serikali yatangaza...





Serikali imewataka maafisa wa jeshi la polisi hapa nchini kutumia mbinu zote za kijeshi na miongozo katika kuhakikisha wanakomomesha mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambayo yamekuwa janga kwa taifa.
Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Ameselima Pereira ameyasema hayo katika tarifa yake iliyosomwa kwa niaba na naibu mkuu wa jeshi la polisi nchini Bw.Abrahaman Kaniki wakati akifunga mafunzo kwa wakaguzi wasaidizi wa jeshi la polisi katika chuo cha taaluma ya polisi Moshi.
Amesema hali ya amani kwa watu wenye ulemavu wa ngozi hapa nchini kwa sasa siyo ya kuridhisha na kuiomba jamii kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika kuwafichua wahalifu wa mauji hayo ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha taluma ya polisi Moshi afande Matanga Mbushi amesema jumla ya wakaguzi 732 walianza mafunzo hayo mwaka jana lakini waliohitimu ni 709 tu na kwamba wakaguzi 23 waliachishwa mafunzo kutokana na utovu wa nidhamu.

Naye mkuu wa wilaya ya Moshi Bw.Novatus Makunga amewataka maafisa hao kufanyakazi kwa weledi na kufuata misingi ya haki za binadamu kwa kuwa wananchi wanategemea sana jeshi la polisi katika suala zima la ulinzi na usalama.

0 comments:

Post a Comment