This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Monday, 13 November 2017

AUAWA KISA KUSAFIRISHA NG'OMBE….

Viongozi wa kijamii katika mji wa Rajasthan nchini India, wanasema mtu mmoja ambaye ni muislam ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaoamini ng'ombe kuwa mungu wao.

ASKARI WALIOBAKA WATOTO WA MIEZI 18 KIZIMBANI DRC…

Wanajeshi 18 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, wamepandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza wakikabiliwa na kesi ya ubakaji wa halaiki wa watoto.

MAHAKAMA YAMHUKUMU LULU MIAKA 2 GEREZANI...

Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemhukumu kwenda jela miaka miwili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia.

Monday, 30 October 2017

BREAKING:VIDEO-LAZARO NYALANDU AJIVUA UBUNGE AHAMA CCM......

Saturday, 21 October 2017

GAMBO ATOA AGIZO KWA MKURUGENZI……

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli kuhakikisha anasimamia ujenzi wa Ofisi za Kata na unakamilika kabla ya mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.

ADAKWA NA POLISI KWA KUBAKA WATOTO 14…


Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia mganga wa kienyeji mkazi wa mtaa wa Minga Daud Idd (74), kwa tuhuma ya kunajisi watoto 14 wenye umri kati ya miaka saba na 12 na kuwasababishia maumivu makali katika sehemu zao za siri.

MWALIMU AJICHINJA KOROMEO HADI KUFA…

Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi, Leonard Mwipugi (29) amejiua kwa kujichinja koromeo akiwa nyumbani kwake.

ZITO KABWE ASEMA MWANACHAMA AMBAE SAFARI IMEMSHINDA ASHUKE MWENYEWE.

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto kabwe, amekaa mbele ya waandishi wa habari kufafanua mambo mbalimbali ikiwemo ishu ya kujivua unachama kwa aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya kampeni na uchaguzi Samsoni Mwigamba.
Tizama video hapo chini juu ya kile alicholizungumza Zitto Kabwe.

WHO LAMTEUWA MUGABE KUWA BALOZI MWEMA WA AFYA

Shirika la afya duniani WHO limemteuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kama 'balozi mwema ' katika kusaidia kukabiliana na magonjwa yaliyosahaulika.

HELIKOPTA YAANGUKA KATIKA ZIWA KENYA…

Ndege moja aina ya helikopta imeanguka katika ziwa Nakuru nchini Kenya muda mfupi baada ya kuondoka katika hoteli moja mjini humo.

Wednesday, 27 September 2017

WANAWAKE RUHSA KUENDESHA MAGARI SAUDIA....

Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametoa idhini ya wanawake kuendesha magari, hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa. Uamuzi huu umefikiwa kutokana na harakati za muda mrefu kwa makundi ya wanawake na haki za bindamu kushinikiza wanawake waruhusiwe kuendesha magari.

TEKSI NDEGE ISIOKUWA NA RUBANI YAZINDULIWA DUBAI…………

Dubai imefanya jaribio la teksi ya kwanza ya ndege isio na rubani ambayo wanatumaini itatumika kama chombo cha uchukuzi mijini.

MWANAMKE WA KWANZA MAREKANI AHITIMU MAFUNZO YA ‘UKOMANDO’ ARDHINI……..

Mwanamke wa Marekani ameweka historia na kuvunja mwiko baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuhitimu mafunzo ya kikosi maalum cha ‘Marine’ nchini humo ambayo yana uwiano na sehemu ya mafunzo ya ukomando yaliyojikita katika mapambano ya ardhini.

Thursday, 7 September 2017

WATU WANNE WAUAWA KWA KUKATWA VICHWA KENYA….

Watu wanne wameuawa kwa kukatwa vichwa vyao katika eneo la Hindi kaunti ya Lamu, Kenya usiku wa kuamkia Jumatano.

KIPINDUPINDU CHAENEA KWA KASI NIGERIA…….

Umoja wa mataifa umesema kwamba ugonjwa wa kipindupindu umeendea kwa kasi kubwa katika kambi za makaazi ya watu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

UTAFITI: MBWA MWITU HUFANYA UAMUZI KWA KUPIGA CHAFYA...

Mbwa mwitu hufanya maamuzi yao kwa kupiga kura kupitia kupiga chafya kwa mujibu wa utafiti mpya.

Monday, 4 September 2017

RUBANI WA JESHI AANGUKA KUTOKA KWENYE HELIKOPTA UBELGIJI……

Wanajeshi wa Ubelgiji wanamtafuta rubani wa helikopta ya jeshi ambaye alianguka kutoka kwa ndege hiyo wakati wa maonesho ya ndege za kivita.

VIDEO: KICHAKA-SAIDA KAROLI FT BELLE 9 & G NAKO..

Leo Septemba 4, 2017 Msanii wa nyimbo za asili nchini Tanzania, Saida Karoli aliyevuma kitambo, na kurudi tena kwa nguvu ya ajabu, ameachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Kichaka’ ambapo katika wimbo huo amewashirikisha Belle 9 pamoja na G Nako.

NJIWA ALIYETUMIWA KUSAFIRISHA MIHADARATI APIGWA RISASI….

Polisi nchini Argentina wamempiga risasi njiwa ambaye alitumiwa kusafirisha mihadarati kwenda gereza moja nchini humo, kwa mujibu wa mamlaka za gereza.

MAHUJAJI 35 WAAGA DUNIA WAKIFANYA IBADA MAKKAH……

Katika Ibada ya Hijja inayofanyika kila mwaka na kutekelezwa na Waislamu nchini Saudi Arabia katika Msikiti Mkuu mji wa Makkah eneo takatifu, Mahujaji 35 wafariki dunia.

Friday, 1 September 2017

TREANDING:UCHAGUZI WA URAIS KENYA WAFUTWA……

Mahakama ya juu nchini Kenya imebatilisha uchaguzi wa urais nchini humo baada ya kujiridhisha kuwa ulikuwa na kasoro nyingi zilizokiuka katiba na utawala wa sheria.

Thursday, 31 August 2017

WATU MAARUFU WADUKULIWA KATIKA MTANDAO WA INSTAGRAM…..

Instagram imegundua dosari katika mfumo wake iliofichua nambari za simu za watu maarufu pamoja na anwani zao kwa wadukuzi wa mitandao.

CHUO CHATUMA DOLA MILIONI MOJA KWA MWANAFUNZI KIMAKOSA AFRIKA KUSINI….

Chuo Kikuu kimoja nchini Afrika Kusini kimesema kwamba kilituma kimakosa jumla ya randi milioni 14 ambazo ni sawa na dola milioni moja za Marekani katika akaunti ya benki ya mwanafunzi mmoja nchini humo.

WANAFUNZI KUFUNZWA KUHUSU NJIA ZA KUTOA TALAKA INDIA…

Shule moja nchini India itaanza kuwafunza wavulana wa Kiislamu njia za kutoa talaka kulingana na sheriza za Kiislamu.

Tuesday, 29 August 2017

VIDEO: KAMANDA MPYA DSM AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA...


Kamanda mpya wa kanda maalum ya Dar es salaam aliyeteuliwa hivi karibuni,mchana wa leo amezungumza na waandishi wa habari kujitambulisaha na kutoa namba yakeya simu.

MAMBO MAZITO USIYOYAJUA JUU YA MATETEMEKO YA ARDHI……

Hadi sasa haijagunduliwa teknolojia ya kuaminika, inayoweza kutabiri kutokea kwa matetemeko ya ardhi popote Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla. Akizungumza mwishoni mwa wiki ofisini kwake mjini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Gabriel Mbogoni alisema teknolojia hiyo haipo popote duniani.

WASIWASI AFRIKA KUSINI BAADA YA VISA VYA ULAJI WA NYAMA YA BINADAMU…..

Hofu imekumba kijiji cha Shayamoya katika jimbo la KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini, baada ya kupatikana kwa maiti ya binadamu iliyonyofolewa myama yote.

LIVE: KESI YA UCHAGUZI KENYA..Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni huko nchni kenya,inaendelea kusikiliwa katika mahakama nchini humo

VIDEO: LISSU, LHRC WAUNGANA KUPINGA KULIPULIWA OFISI YA MAWAKILI…………

Tundu Lissu na Kituo cha Haki za Binadamu zimeungana kwa pamoja katika kupinga kitendo cha kuvamiwa na kulipuliwa Ofisi za IMMMA Advocates.

WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI…..

Waalimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu shuleni hapo.

MUUGUZI ADAIWA KUHUSIKA KATIKA VIFO VYA WATU 84 UJERUMANI………….

Muuguzi mmoja anayetumikia kifungo cha maisha jela kwa kuwauwa wagonjwa wawili kaskazini mwa Ujerumani, sasa anashukiwa kuhusika na visa 84 vya mauaji.

HUYU NI MTU ANAYEFUNZA KOMPYUTA KUTAMBUA HARUFU…

Raia wa Nigeria Oshi Agabi amezindua kompyuta zinazotumia neva za panya katika kongamano la kiteknolojia la TEDGlobal linaloendelea nchini Tanzania.

Monday, 28 August 2017

VIDEO:POLISI WAZUNGUMZA KUHUSU KULIPULIWA OFISI ZA MAWAKILI…

Kufutaia tukio la kulipuliwa kwa ofisi za immma advocates, ambazo inaelezwa kuwa hutumiwa pia na wakili fatma karume.

MHASIRIWA WA UBAKAJI INDIA, MWENYE UMRI WA MIAKA 13 AIOMBA MAHAKAMA KUAVYA MIMBA….

Wazazi wa msichana mwenye umri wa miaka 13 mhasiriwa wa matendo ya ubakaji kutoka mji wa Mumbai huko India, wamekwenda katika mahakama kuu ya nchi hiyo, kuomba idhini ya kuavya mimba aliyo nayo binti wao.

UPINZANI WARUHUSIWA KUKAGUA MITAMBO YA TUME YA UCHAGUZI KENYA………..

Mahakama ya Juu nchini Kenya imeukubalia muungano wa upinzani nchini humo National Super Alliance (Nasa) kupekua sava zilizotumiwa na tume ya uchaguzi nchini humo wakati wa uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti.

HOMA YA NGURUWE TISHIO NCHINI INDIA…


Mlipuko wa Homa ya Nguruwe ulioikumba India umesababisha vifo vya watu 1,094, kwa kipindi cha miezi minane iliyopita huku ikisemekana kuwa ugonjwa huo ni hatari zaidi na unasambaa kwa kasi.

Friday, 25 August 2017

MKUU WA SAMSUNG AFUNGWA JELA MIAKA 5….

Mahakama nchini Korea Kusini imemhukumu bilionea anayetarajiwa kurithi kampuni Samsung Lee Jae-yong kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya utoaji rushwa.

MFUNGWA AUAWA KWA KUTUMIA SUMU MPYA FLORIDA, MAREKANI…..

Mzungu mtetea ubabe wa wazungu ambaye akliwaua watu kwa sababu ya asili yao miaka 30 iliyopita ameuawa kwa kudungwa sindano yenye sumu.

MADAKTARI MBARONI KWA KUUZA VIUNGO VYA BINADAMU…..

Serikali ya Misri imewakamata madaktari ambao wanatuhumiwa kuhusika na mtandao wa biashara ya kuuza viungo vya binadamu.

WENYE VVU WAKITUMIA VIZURI ARVS HAWAWEZI KUAMBUKIZA...

Wenye Virusi Vya Ukimwi (VVU) wanaotumia dawa za kufubaza virusi (ARVs), wamethibitika kitaalamu kuwa wakitumia dawa hizo kwa uaminifu bila kukatisha dozi, hawawezi kuwaambukiza watu wengine kwa kujamiiana.

Thursday, 24 August 2017

VIDEO: KITUO CHA SHERIA CHATOA TAMKO LA KUHUSU UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI….

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, leo kimekutana na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,na kutoa Tamko kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini yanayosababisha uvunjifu wa haki za binadamu.

MWANAFUNZI AFARIKI KATIKA AJALI YA TRENI NA DALADALA MOROGORO…

Mtu mmoja amefariki na wawili wamejeruhiwa baada ya gari ya abiria kugonga treni eneo la Tanesco Morogoro.

RAIS AIDHINISHA HIFADHI KUBWA ITUMIWE KWA UCHIMBAJI MADINI…

Serikali ya Brazil imefutilia mbali hifadhi kubwa ya taifa katika eneo la Amazon ili kutoa fursa ya uchumbaji wa madini katika eneo hilo.

SAMSUNG WAZINDUA TOLEO JIPYA LA GALAXY…

Kampuni ya simu za mkononi ya Sumsung, imezindua simu yake mpya ya Galaxy Note 8, ambayo ni ya kisasa zaidi na yenye ushindaji zaidi katika soko.

Tuesday, 22 August 2017

INDIA YAPIGA MARUFUKU TALAKA YA KUTAMKA TU…

Mahakama ya juu nchini India imeamua kuwa talaka ya mara moja katika dini ya kiislamu ni kinyume na katiba, uamuzi ambao umekuwa ni ushindi mkubwa kwa haki wanawake.

WASHTAKIWA KWA KULA NYAMA YA BINADAMU…..

Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.

Saturday, 19 August 2017

NEW VIDEO:ROMA & STAMINA-HIVI AMA VILE

Roma na Stamina kupitia umoja wao ‘Rostam’ ameachia video ya ngoma yao mpya ‘Hivi Ama Vile’, video imeongozwa na Nicklass, audio ni Mr. T Touch.

MWANAMKE MTANZANIA AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA INDIA….

Mamlaka katika Mji wa New Delhi, India zimearifu kuwa zimewakamata Wanawake wawili wa Kiafrika baada ya kuwakuta na Dawa za Kulevya aina ya cocaine yenye thamani ya Dollar Milioni 6 za Marekani.

POLISI WAANZISHA MSAKO MKALI KUWATAFUTA WALIOMUUA WAYNE LOTTER……….

Jeshi la Polisi nchini Tanzania linaendelea na msako mkali kuwatafuta watu waliompiga risasi na kumuua Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation, Wayne Lotter jijini Dar es Salaam juzi.

ZAIDI YA WATOTO 35,000 WAPATA CHANJO YA POLIO SYRIA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la afya duniani WHO kwa kushirikiana na wadau wengine wamekamilisha duru ya kwanza ya kampeni ya chanjo kukabiliana na mlipuko wa karibuni wa polio nchini Syria.