Mwanamke wa Marekani ameweka historia na kuvunja mwiko baada ya kuwa
mwanamke wa kwanza kuhitimu mafunzo ya kikosi maalum cha ‘Marine’ nchini humo
ambayo yana uwiano na sehemu ya mafunzo ya ukomando yaliyojikita katika
mapambano ya ardhini.
Mwanamke huyo ambaye hakupenda
jina lake litajwe, amehitimu mafunzo hayo Jumatatu katika eneo la Quantico,
Virginia.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizotolewa na Jeshi la Marekani, mwanamke huyo amepewa kazi ya kwanza ya
kuongoza vikosi 40 vya jeshi vyenye nguvu.
Kamanda wa vikosi maalum vya
jeshi la Marekani, Jenerali Robert Neller ametweet picha ya mwanamke huyo na
kueleza kuwa anajivunia kuwa naye pamoja na viongozi wenzake.
Kwa
mujibu wa BBC, kati ya wanajeshi 131 walioshiriki mafunzo hayo maalum, ni
wanajeshi 88 pekee waliohitimu. Asilimia 10 ya wanajeshi wanaopangiwa mafunzo
hayo hushindwa katika siku ya kwanza.
Machi
2016 aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama alifungua milango ya nafasi za
jeshi kwa wanawake na kutaka wapewe nafasi hata kwenye vikosi maalum vya juu.
Hata
hivyo, utafiti uliofanywa ulionesha kuwa wanajeshi wengi wa Marekani wanapinga
wanawake kujumuishwa kwenye oparesheni za vikosi maalum.
0 comments:
Post a Comment