Katika Ibada ya Hijja inayofanyika kila mwaka na kutekelezwa na
Waislamu nchini Saudi Arabia katika Msikiti Mkuu mji wa Makkah eneo
takatifu, Mahujaji 35 wafariki dunia.
Taarifa hizo zimetolewa rasmi
na Wizara ya Afya nchini Misri, ambapo imesema kuwa siku ya kwanza ya ibada
hiyo imepoteza Mahujjaji 35 kutokana na sababu ya uchovu na umri mkubwa.
Afisa mmoja wa Wizara hiyo,
Ahmed el Ansary, amesema umri wa Mahujaji waliofariki ni kati ya miaka 60 hadi
85.
Katika Ibada hiyo ya Hijja
mwaka huu zaidi ya Mahujaji milioni mbili wamehudhuria wakiwemo milioni 1.8
kutoka nje ya nchi.
Mahujaji hao wamekuwa
wakifanya utaratibu huo wakifuata nyayo za Mtume wao Muhammad, aliyefanya utaratibu
huo wa ibada miaka 1400 iliyopita.
0 comments:
Post a Comment