Wanajeshi
wa Ubelgiji wanamtafuta rubani wa helikopta ya jeshi ambaye alianguka kutoka
kwa ndege hiyo wakati wa maonesho ya ndege za kivita.
Wanajeshi watatu waliruka kutoka kwa
helikopta hiyo aina ya Agusta A-109 wakiwa na parachuti, lakini rubani huyo na
msaidizi wake hawakuwa na parachuti, vyombo vya habari Ubelgiji vimeripoti.
Taarifa zinasema rubani msaidizi
aliwasaidia wanajeshi hao watatu kuruka nje, lakini aliporudi kutazama kiti cha
rubani akashangaa kupata rubani hayupo.
Alichukua usukani na kuanza
kuiongoza ndege.
Maonesho hayo yalikuwa yakifanyika
katika eneo la Amay, karibu na mji wa Liège.
Rubani huyo alianguka mita mia kadha
kutoka angani.
Sababu ya rubani huyo kuanguka bado
haijulikani.
0 comments:
Post a Comment