Mbwa
mwitu hufanya maamuzi yao kwa kupiga kura kupitia kupiga chafya kwa mujibu wa
utafiti mpya.
Utafiti huo wa pamoja uliofanywa
na wasomi kutoka Swansea, Australia na Marekani ulifuatilia mbwa mwitu walio
kwenye hatari ya kuangamia nchini Botswana.
Waligundua kuwa mbwa walitumia chafya kuamua wakati
wanaelekea kuwinda baada ya kufanya mikutano inayofahamika kuwa mikutano wa
kijamii.
Awali ilikuwa ikifikiriwa kuwa mbwa hao ambayo ni familia
ya wanyama walio kwenye hatari zaidi ya kuangamia duniani, walikuwa wakipiga
chafya ya kawaida.
Lakini wakati watafiti walirekodi
mikutano 68 ya mwa mwitu waligundua kuwa wakati walipiga chafya zaidi walikuwa
wakiondoka na kuanza wa kuwinda.
Dr King anasema kuwa chafya hiyo ni lazima ifike kiwango
fulani kabla ya wao kuamua kufanya kitu.
Pia uutafiti huo uligundua baadhi
ya chafya huwa na uzito kuliko zingine.
0 comments:
Post a Comment