This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday 28 February 2017

WATALII 2 KUPELEKWA MWEZINI 2018...

Safari hiyo itafanyika 2018 kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SpaceX Elon Musk, alieongezea kwamba watalii hao tayari wamelipa kiasi fulani cha fedha.

VYOMBO VYA PLASTIKI CHANZO CHA SARATANI….

Imebainika kuwa vifaa vya plastiki hutengenezwa kwa kemikali zaidi ya 200, hivyo kuwa chanzo cha aina 100 za ugonjwa wa saratani.

Monday 27 February 2017

MAJAJI WAICHARUKIA SERIKALI KESI YA LEMA

Mwenyekiti wa kikao cha jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, kinachoendelea Arusha, Bernard Luanda, leo amegeuka mbogo kwa wanasheria wa serikali kwa kitendo cha kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhamana kwa lengo la kumyima haki.

WAZIRI KIGWANGALLA AAHIRISHA ‘PRESS CONFERENCE’ YA KUTANGAZA WANAOJIHUSISHA NA USHOGA.

Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangalla, amesema kuwa hawatokuwa na press conference ya kutangaza majina ya mashoga wanaojiuza na kujitangaza mitandaoni.
Waziri huyo aliahidi kutangaza majina na mashoga ambao wanatuhumiwa kujiuza mtandaoni kinyume na sheria.

Jumatatu hii waziri huyo alitoa taarifa ya kuahirisha kutaja majina hayo kwa madai kuna matatizo ya kiufundi.

“Tunaomba radhi hatutokuwa na press conference kuhusu kutangaza majina ya mashoga wanaojiuza mitandaoni kwa sababu za kiufundi!,” alitweet Kingwangala.

Sunday 26 February 2017

WAVUTAJI MBEYA WALALAMIKA BANGI KUADIMIKA MTAANI (AUDIO)

Wavutaji mkoani Mbeya wamelalamika bangi kuadimika mtaani tangu vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya ishike kasi nchi nzima. Mmoja wa wavutaji mashuhuri wa mmea huo ambaye amedai kuanza kuvuta akiwa na darasa la 6, amedai kuwa ili kuipata inawalazimu kwenda nje ya mji kwakuwa wauzaji wakubwa wamekimbia mjini. Msikilize zaidi hapo chini.

MSICHANA ANAYETUHUMIWA KUHUSIKA NA MAUAJI YA KIM JONG-NAM ADAIWA KULIPWA DOLA 90 SAWA TSH 200,000

Mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, anasema alilipwa dola 90 sawa tsh 200,000, kushiriki katika kile alichofikiri, ni kitendo cha mzaha.

Thursday 23 February 2017

WEMA SEPETU AHAMIA CHADEMA, AUNGANA NA MBOWE MAHAKAMANI.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo na chama hicho akiwemo Miss Tanzania wa zamani na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia .waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu.
Wema pamoja mama yake, leo aliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho kwenye mahakama kuu jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo aliyeshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.

VIDEO: KUNA COLABLE YA ALLY KIBA NA YVONNE CHAKA CHAKA INAKUJA...

Tizama  simulizi hapo chini kuhusu collabo hiyo ya Yvonne Chakachaka na Alikiba.

Wednesday 22 February 2017

NASA WATATANGAZA NINI KUHUSU MFUMO WA JUA?

Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) leo linatarajiwa kutangaza ugunduzi "mkubwa" kuhusu mambo yaliyomo "nje ya mfumo wetu wa jua".
Hafla ya kutangaza ugunduzi huo itapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga ya Nasa na katika mtandao wa shirika hilo mwendo wa saa kumi na mbili jioni (GMT) ambazo ni sawa na saa tatu Afrika Mashariki Jumatano jioni.

JALADA LA MASOGANGE LAKWAMA KWA AG.

Msanii  maarufu anayepamba  video za wasanii wa muziki wa bongo Fleva (Video Queen) Agnes Gerald maarufu Masogange ameendelea kusota rumande, huku jalada lake likiendelea kuwa mikononi mwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

KASHMIR:MARUFUKU MATUMIZI YA ANASA…..

Serikali ya Jimbo la Kashmir nchini India imeweka zuio dhidi ya gharama za anasa.
Wazazi wa bibi harusi watapigwa marufuku kualika zaidi ya wageni mia tano, au mia nne ikiwa mtoto wa kiume atakuwa anaoa.

WABUNGE WAIDHINISHA KILIMO CHA BANGI UHOLANZI.

Bunge la chini nchini Uholanzi, limeidhinisha kuhalalishwa kwa kilimo cha bangi.
Mswada huo ulioidhinishwa utawakinga wakulima wa bangi, ambao wanatimiza masharti fulani dhidi ya kuadhibiwa.

Tuesday 21 February 2017

WANAWAKE WAPIGWA MARUFUKU KUSAFIRI PEKE YAO LIBYA…

Maafisa wa kijeshi wanaodhibiti eneo la mashariki mwa Libya, wametangaza marufuku kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 60 ya kuwazuia kusafiri nje ya nchi wakiwa peke yao.

MUGABE ASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 93…

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, kiongozi wa taifa mwenye umri wa juu zaidi duniani kwa sasa, ametimiza miaka 93.

MZEE AISHI CHINI YA MTI KWA MIAKA 15

Mzee wa miaka 72 ambaye alikuwa Ofisa Elimu Mkoa wa Tanga mwaka 1975, John Kihendo aliyestaafu mwaka 1989, ameamua kuishi chini ya mti kwa muda wa miaka 15 kwa madai kuwa anaitafuta haki ya shamba lake lenye ukubwa wa hekari sita lililoko kata ya Magomeni jijini Tanga.

Monday 20 February 2017

VIDEO: WYRE-LION

After giving us a top notch music video shot in Atlanta featuring Dj Protege some time back, Wyre has released a heartfelt jam ‘Lion’ that expresses his love for his son. Lion shows a softer side of the artist.

The video is personal but mostly of sentimental value. Thee dancehall artist did it again.
“The song is about my son & what he means to me” – Says Wyre
The Jam was Produced by Andre Ricardo Bailey(Tenament Yard Records) Engineered by Mwax The Herbalist,Directed by Cream Visions and Promoted by Muziki Kenya

Saturday 18 February 2017

TID FT FID Q - MAISHA YA JELA (OFFICIAL AUDIO)


This majestic song was recorded back in 2007, astonishingly, 3 days after vacating those jail bars and bolts.

What one must reflect on is the fact that TID wouldn't have been out of those daunting shackles if it wasn't for the pardon from the former Tanzanian president, His honorable 

MUGABE ANAWEZA KUPIGIWA KURA AKIWA MAITI..

Grace Mugabe na mumewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Mke wa Rais mkongwe wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema kuwa mumewe ni mashuhuri sana hivi kwamba anaweza kupigiwa kura hata akiwa maiti.

SIMU YA ADOLF HITLER KUPIGWA MNADA MAREKANI.

Simu iliokuwa ikitumiwa na kiongozi wa Wanazi Adolf Hitler kupigwa mnada Marekan
Simu iliyokuwa ikitumiwa na Adolf Hitler wakati wa vita vikuu vya pili vya Dunia itapigwa mnada nchini Marekani mwisho mwa juma hili.

Friday 17 February 2017

WAGONJWA SASA KUWEKEWA MOYO BANDIA...

Nchini Marekani kila baada ya dakika 10 mtu mmoja huwekwa kwenye foleni ya watu wanaosubiri kuwekewa moyo mpya ili kuweza kuendelea kuishi.

NEW VIDEO: DAVIDO-IF

Davido Mwimbaji staa kutokea Nigeria ambaye ameshawahi kuja kutumbuiza Tanzania, tayari mpaka sasa anazo hits kadhaa zilizofika mpaka kwenye Top10 za Radio na TV Tanzania.
Itazame video hiyo hapa chini.

VIDEO MPYA:ALIKIBA KATULETEA VIDEO YA ‘AJE REMIX’

Mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba ametuletea video mpya ya ‘Aje remix’aliyomshirikisha M.I kutoka Nigeria ambapo imesimamiwa na Director Meji Alabi, ukishaitazama usisahau kuacha comment yako mtu wa nguvu.

SIMU ZA NOKIA 3310 KUREJEA…?

Kuna taarifa kwamba huenda simu muundo wa Nokia 3310 zikazinduliwa upya na kuanza kuuzwa tena baadaye mwezi huu.

Thursday 16 February 2017

UBUNGE WA BULAYA BADO WA NG’ANG’ANIWA…

Wapiga kura wanne wa Jimbo la Bunda waliofungua shauri kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita wameendelea kumng’ang’ania mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya kwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutupa maombi yao.

ZITTO ANENA KUHUSU KUFUNGIWA KWA WIMBO (I M SORRY JK ) WA NIKKI MBISHI

Wimbo mpya wa rapper Nikki Mbishi, I’m Sorry JK umefungiwa.
Uamuzi huo umekuja saa chache baada ya rapper huyo kuitwa na Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA Jumatano hii kujielezea kuhusiana na wimbo huo. Kupitia Instagram, Nikki amewaonya watu dhidi ya kuusambaza wimbo huo kwakuwa mkono wa sheria utawaangukia.
“Naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia,” ameandika kwenye Instagram. “Napokea simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakaohitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA,naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili,” ameongeza.
Pia ameonya, “Kwa yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru popote duniani na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa,hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria. Asanteni sana,naomba msubiri ujio wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k.”

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook: Serikali imepiga marufuku wimbo wa msanii Nikki Mbishi. Wallah nilidhani ni utani kumbe Kweli? Serikali hii inachoogopa ni nini? Dah kua uyaone.”
USIKILIZE WIMBO HUO HAPA CHINI

VIDEO: NAY WAMITEGO-MUDA WETU {OFFICIAL VIDEO HD NEW SONG}

Anaitwa Ney wa Mitego ametuletea tena mziki mzuri kwenye Runinga zetu,chukua time yako kiduchu kuikodolea macho hii video yake mpya hapa chini.

ZAIDI YA WATOTO 25,000 KUPATA KANSA KILA MWAKA..

Katika Kuadhimisha Siku ya Saratani duniani, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Asasi ya Marafiki wa Watoto wenye Saratani Tanzania (FoCC) Janeth Manoni, amesema kwa sasa ugonjwa huo umekuwa tishio kwa watoto nchini, ambapo inakadiriwa zaidi ya watoto 25,000 hupata ugonjwa huo kila mwaka.

WALIOONGOZA MGOMO WA MADAKTARI WAACHIWA HURU

Mahakama ya Rufaa nchini Kenya imeamuru kuachiliwa huru mara moja kwa viongozi wa chama cha wauguzi na madaktari nchini humo waliohukumiwa kifungo cha mwezi mmoja jela.

ALIYETEULIWA NA TRUMP KUWA WAZIRI AJITOA..

Andrew Puzder aliyekuwa ameteuliwa na Rais wa Marekani Donald Trump kuwa waziri wa masuala ya wafanyakazi, amejiondoa muda mfupi kabla ya kuhojiwa na wabunge.

Wednesday 15 February 2017

VIDEO: KING KIBA ATUA AFRIKA KUSINI KUANZA ZIARA YAKE

Mshindi wa tuzo ya MTV EMA 2016, Alikiba ametua nchini Afrika Kusini tayari kwa ziara yake ya kwanza nchini humo.
Alikiba (nyuma) akiwa na meneje wake Seven Mosha nchini Afrika Kusini)Wakati akitangaza kwa mara ya kwanza ziara hiyo, Alikiba aliandika, “Happy New Year. It’s time to meet my fans across the world. I start with South Africa in February 2017! .
 KING KIBA LIVE ON TOUR IN SOUTH AFRICA

MAKAMANDA WA MIKOA WATAKIWA KUONGEZA NGUVU VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA…

Katika kuhakikisha kuwa biashara haramu ya dawa za kulevya inakomeshwa hapa nchini na kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya kupambana na tatizo la dawa

INDIA YAWEKA REKODI KWA KURUSHA SATELAITI 104…

India imeweka rekodi mpya kwa kuwa taifa lililorusha setilaiti nyingi angani kwa wakati mmoja baada ya kurusha setilaiti 104 kwa pamoja.

Tuesday 14 February 2017

MAREKANI YASEMA KOREA YA KASKAZINI NI TATIZO..

Rais wa Marekani, Donald Trump ameizungumzia Korea ya Kaskazini baada ya kitendo chake cha hivi karibuni cha kurusha kombora lenye uwezo wa kubeba silaha za kinyuklia kwamba nchi hiyo ni hatari kwa usalama wa dunia.

MGODI MWINGINE WAPOROMOKA MARA..


Takribani mwezi mmoja sasa tangu wachimbaji 15 wafukiwe na kifusi Nyarugusiu Wilayani Geita, balaa jingine la aina hiyo limetokea wilayani Butiama mkoani Mara, katika mgodi wa Buhemba ambapo watu 11 wameokolewa shimoni wakichimba dhahabu.

Video: Mwaki ft G Van-Nishike Mkono


Msanii wa muziki, Mwaki ambaye ni mlemavu wa macho, ameachia video ya wimbo wake ‘Nishike Mkono’ akiwa amemshirikisha G Van. Video ya wimbo huyo imeongozwa na director Flex Montage for Urban Motion Films

AMUUA MFANYAKAZI AKIDHANI NI NGIRI AFRIKA KUSINI..

Watu nchini Afrika Kusini wamegadhabishwa, kufuatia taarifa za mwanamme mmoja, ambaye analaumiwa kwa kumuua kwa kumpiga risasi mfanyakazi wa shamba, akidhani kuwa mtu huyo ni ngiri.

MAHARUSI WALIOTUMIA DOLA PEKEE WAANDALIWA HARUSI YA KIFAHARI KENYA

Maharusi waliowasisimua wengi baada ya kutumia Sh100 pekee za Kenya kugharimia harusi, wameandaliwa sherehe ya harusi ya kufana jijini Nairobi.

PLAYBOY KUCHAPISHA TENA PICHA ZA UTUPU..

Jarida la Playboy limetangaza kwamba litaanza kuchapisha tena picha za utupu, na kubatilisha uamuzi wa awali uliotolewa mwishoni mwa mwaka jana.

KWA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI..

Mahakama ya Juu nchini India imefuta leseni za madaktari 634 ambao wamejipata kwenye sakata ya wanafunzi kutumia udanganyifu kujiunga na vyuo vya mafunzo ya udaktari katika jimbo la Madhya Pradesh.

WATU 80 MBARONI KWA DAWA ZA KULEVYA ARUSHA…

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limenasa watuhumiwa 80 wanaojihusisha na mtandao wa dawa za kulevya, akiwemo askari Polisi mmoja mwenye namba 6978 Koplo zakayo ambaye anashikiliwa kwa mahojiano.

Monday 13 February 2017

VIONGOZI WA MADAKTARI KENYA WAFUNGWA JELA..

Mahakama ya masuala ya wafanyakazi nchini Kenya, imewahukumu viongozi saba wa chama cha wahudumu wa afya (KMPDU) kufungwa jela mwezi mmoja.

WAFIKA POLISI KUOMBA WAPEWE DAWA ZA KULEVYA........

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya waathirika wa dawa za kulevya maarufu kwa jina la ‘mateja’ wamefika makao makuu ya polisi mkoa wa Mbeya kuomba wapewe dawa hizo kidogo kwani zimeadimika mtaani.

Friday 10 February 2017

HIVI NDIVYO DAWA ZA KULEVYA ZINAVYOHARIBU UBONGO.

Watafiti wamefanya chunguzi mbalimbali kwa kutumia wanyama kama mfano wa kazi amilifu za ubongo wa binadamu ili kufafanua michakato ya kimsingi ya dawa za kulevya katika ubongo. Mada hii ya kushangaza inashirikisha maeneo kadhaa za ubongo na mabadiliko ya sinapsi au mageuko ya neva, ambayo hutokea katika maeneo hayo. Athari kali

MAGARI 200 YA MSAFARA WA RAIS YATOWEKA GHANA…

Serikali mpya nchini Ghana inayatafuta magari 200 yaliyokuwa yakitumiwa na afisi ya rais ambayo yanadaiwa kutoweka, msemaji wa rais amesema.

WATU WATANO WAAMBUKIZWA UKIMWI HOSPITALINI CHINA..

Hospitali moja nchini Uchina imekiri kwamba watu watano waliambukizwa virusi vinavyosababisha Ukimwi hospitalini humo kimakosa.

MKALIMANI FEKI WA MTALII ATIWA NGUVUNI

Mwongoza Watalii (Guide), ambaye anadaiwa kupotosha tafsiri ya matamshi ya mtalii aliyekuwa amemaliza kutembelea Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), ametiwa mbaroni.
Video ya mwongoza watalii huyo, ilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, na kuzua taharuki katika sekta ya Utalii nchini,huku wadau wengi wakitaka asakwe na kukamatwa.
Katika video hiyo, mtalii huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, anaonekana akisema safari yake nchini Tanzania imekuwa nzuri na watanzania aliokutana nao walikuwa ni watu wenye upendo.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu leo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema mara baada ya kuona video hiyo kwenye mitandao aliagiza akamatwe mara moja.

“Nilitoa maagizo jana (juzi) usiku atafutwe na akamatwe na taarifa nilizopewa leo ni kuwa ameshakamatwa kwenye gate (lango) la Nabi Serengeti na yuko rumande kule Mugumu”alisema.

Thursday 9 February 2017

MERRY YOU YA DIAMOND FT NEYO IMEKOPIWA KUTOKA KWENYE WIMBO WA KCEE NIGERIA



VIDEO: KHULI CHANA FT. CASSPER NYOVEST & MDB – ALL HAIL

Rapper kutoka Africa Kusini Khuli Chana ametoa video mpya ya wimbo “All Hail”, amewashirikisha Cassper Nyovest na MDB, itazame hapa.

RWANDA YAKIPITISHA KISWAHILI KUWA LUGHA RASMI YA TAIFA

Wabunge nchini Rwanda jana waliipitisha sheria ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya rasmi ya taifa hilo.
Kiswahili kitaungana na Kinyarwanda, Kiingereza na Kifaransa, kama lugha ya nne rasmi ya nchi hiyo.
Kwa sasa lugha hiyo itatumika kwenye shughuli za uongozi na kitaonekana kwenye baadhi ya nyaraka za kiofisi.

Lugha hiyo pia itaingia kwenye mitaala ya elimu.