Tuesday 14 February 2017

WATU 80 MBARONI KWA DAWA ZA KULEVYA ARUSHA…

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limenasa watuhumiwa 80 wanaojihusisha na mtandao wa dawa za kulevya, akiwemo askari Polisi mmoja mwenye namba 6978 Koplo zakayo ambaye anashikiliwa kwa mahojiano.


Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo, amesema askari huyo amekamatwa kwa sababu ya kubambikizia watu bangi, na kuanza kuwatisha ili apate rushwa kitendo ambaho kinyume cha sharia.

Mkumbo amesema katika msako wa dawa za kulevya, hakuna mtu atakayebaki salama hata kama ni askari.
Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa ndani ya mwezi huu, walipoanza msako wa madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali ya Wilaya zake na Mkoa wa Arusha.

0 comments:

Post a Comment