Wednesday, 1 February 2017

MPANGO ATAJA KINACHOKWAMISHA UKUAJI WA UCHUMI…..

Serikali imesema matokeo ya ukuaji wa pato la taifa kwa mwaka 2016 yalitarajiwa kuwa 7.2% lakini kwa uchambuzi uliofanywa na serikali kwa kushirikiana na shirika la fedha duniani IMF unaonesha kuwa ukuaji wa uchumi uliotegemewa unaweza usifikiwe.


Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mipango wakati akiwasilisha kauli ya serikali bungeni kuhusu mwenendo wa hali ya uchumi wa taifa ilivyo na kuongeza kuwa matarajio ya sasa ni kufikia ukuaji wa wastani wa asilimia 7.0.

Amesema kuzorota kwa ukuaji wa uchumi nchini umetokana na kwamba nchi za Jumuiya ya Ulaya na China ambao ni wabia wakubwa wa Tanzania kibiashara na uwekezaji ndiyo kumechangia kupunguza matarajio ya awali ya kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Wakati huohuo Dkt. Mipango amesema uamuzi wa serikali kuzitaka taasisi za umma kufungua akaunti za mapato benki kuu ni sababu pia ya kupungua kwa ukwasi katika uchumi wa nchi.


Tizama vieo hapo chini..

Reactions:

0 comments:

Post a Comment