Thursday, 9 February 2017

TUNDU LISSU AGOMA KULA, ADAI MPAKA AFIKISHWE MAHAKAMANI..

Wakati Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akigoma kula hadi afikishwe mahakamani, wakili wake amepeleka maombi Mahakama Kuu kuomba apewe dhamana baada ya polisi kuendelea kumshikilia kwa siku ya tatu.

Wakili wa mbunge huyo Peter Kibatala amesema kuwa, mteja wake amefikia hatua hiyo, baada ya Jeshi la Polisi linalomshikilia kumnyima dhamana bila sababu.
Kibatala amesema hakuna sababu za msingi za kumnyima dhamana mteja wake, na tangu jana Lissu hajala na amesema hatakula hadi afikishwe mahakamani.
Amesema mteja wao analalamikia kuanzia ukamatwaji wake ulipoanza, alipokamatwa eneo la Bunge bila Spika kuwa na taarifa.

Kibatala amesema polisi waliokwenda kumkamata aliwatambua njiani na alikamatwa bila kuwapo kibali cha kukamata (arrest warrant)

Reactions:

0 comments:

Post a Comment