Mahakama ya Rufaa nchini Kenya
imeamuru kuachiliwa huru mara moja kwa viongozi wa chama cha wauguzi na
madaktari nchini humo waliohukumiwa kifungo cha mwezi mmoja jela.
Viongozi hao saba walifungwa Jumatatu
wiki hii baada ya kupatikana na hatia ya kutotii amri ya mahakama ya kuwataka
kumaliza mgomo wa madaktari ambao umedumu kwa zaidi ya miezi miwili sasa.
Viongozi hao
wametakiwa kuhakikisha suluhu ya mgomo huo inapatikana katika kipindi cha siku
saba.
Mazungumzo ya
kutafuta suluhu yataongozwa na Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) na Tume ya
Taifa ya Haki za Binadamu (KNHCR).
Madaktari
wamekuwa wakiitaka serikali kuheshimu makubaliano ya mwaka 2013 ya kuwaongezea
mishahara na kuboresha mazingira ya utendaji kazi hospitalini
Wamekataa
mshahara walioongezewa na serikali wa asilimia 40 wakisema kuwa ni wa chini
kuliko ule walioafikiana mwaka 2013.
0 comments:
Post a Comment