Thursday 23 February 2017

WEMA SEPETU AHAMIA CHADEMA, AUNGANA NA MBOWE MAHAKAMANI.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo na chama hicho akiwemo Miss Tanzania wa zamani na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia .waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu.
Wema pamoja mama yake, leo aliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho kwenye mahakama kuu jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo aliyeshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.

0 comments:

Post a Comment