Thursday, 2 February 2017

MBWA ALIYEMUUMA NA KUMUUA MTOTO WA RAIS BARROW AUAWA….

Rais Adama Barrow
Mbwa aliyemuuma na kumuua mtoto wa rais wa Gambia Adama Barrow ameuawa.
"Tuliamua kuwa haikuwa vyema kumruhusu mbwa huyu kuendelea kuzururu barabarani.Tulimfanyia uchunguzi na kubain ikuwa hakuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa," taarifa kutoka wizara ya kilimo zilisema.
Mtoto huyo wa umri wa miaka minane Habibu Barrow, aliripoptiwa kuaga dunia akiwa njiani kuenda hospitalini eneo la Manjai karibu na mji mkuu wa Gambia Banjul.
Bwana Barrow alishinda uchaguzi wa rais mwaka uliopita lakini rais aliyekuwa madarakani wakati huo Yahya Jammeh, akakataa kuachia madaraka.
Hata hivyo Jammeh aliondoka Gambia mwezi uliopita baada ya nchi za kanda kusema kuwa zilikuwa zimepanga kumuondoa madarakani kwa nguvu.

Barrow hakuhudhuria mazishi ya mwanawe kwa sababu alishauriwa kusalia nchini Senegal kwa usalama wake wakati huo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment