Serikali
ya Jimbo la Kashmir nchini India imeweka zuio dhidi ya gharama za anasa.
Wazazi wa bibi harusi watapigwa
marufuku kualika zaidi ya wageni mia tano, au mia nne ikiwa mtoto wa kiume
atakuwa anaoa.
Idadi ya aina ya vyakula kwenye
sherehe itakuwa saba, huku mziki wa sauti ya juu na fataki vitapigwa marufuku.
Serikali ya kashmir imesema
imechukua hatua hiyo, baada ya kuwepo kwa malalamiko ya watu kuhusu matumizi
makubwa wakati wa sherehe na kelele zinazowakera wengine.
Amri hizo zitaanza kufanya kazi
mwezi Aprili mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment