Serikali
mpya nchini Ghana inayatafuta magari 200 yaliyokuwa yakitumiwa na afisi ya rais
ambayo yanadaiwa kutoweka, msemaji wa rais amesema.
Chama tawala kilihesabu magari hayo mwezi mmoja, kabla ya
kuingia madarakani baada ya kupata ushindi uchaguzini mwezi Desemba mwaka jana.
Imekuwa kawaida kwa baadhi ya maafisa wa serikali
inayoondoka kutorejesha magari ya serikali, na hulazimu serikali mpya kuyatwaa
kwa nguvu nchini Ghama.
Waziri mmoja katika serikali iliyoondoka ya John Mahama,
hata hivyo amesema kuenezwa kwa habari kwamba wenzake walitekeleza uhalifu ni
makosa.
Aliyekuwa waziri wa usalama Omane Boamah amewaambia wana
habari kuwa, hiyo ni mbinu inayotumiwa na serikali mpya kuipa sababu za kununua
magari mapya.
Kituo cha redio cha Citi FM nchini Ghana kimeripoti
kwamba rais amelazimika kutumia gari aina ya BMW lililoundwa miaka 10 iliyopita,
kutokana na kutorejeshwa kwa magari hayo.
Alipokuwa anatoa taarifa yake Bw Arhin alifichua kwamba
afisi ya rais ilifaa kuwa na magari zaidi ya 300 lakini hakueleza magari hayo
hutumiwa vipi.
0 comments:
Post a Comment