Mzee wa miaka 72 ambaye alikuwa Ofisa Elimu Mkoa wa Tanga mwaka
1975, John Kihendo aliyestaafu mwaka 1989, ameamua kuishi chini ya mti kwa muda
wa miaka 15 kwa madai kuwa anaitafuta haki ya shamba lake lenye ukubwa wa
hekari sita lililoko kata ya Magomeni jijini Tanga.
Hivyo anaiomba serikali kumaliza mgogoro wa shamba hilo uliodumu
kwa zaidi ya miaka saba ili aweze kapata haki yake na hatimaye ajenge makazi ya
kudumu na familia yake.
Mzee alizungumza
na kusema baada ya Wapimaji kuja eneo hilo walidai linatakiwa kutumika kama
kituo cha jamii ‘(Community Centre)’ hivyo mwaka 2004 alipewa fidia
kidogo ambayo haiendani na hilo eneo.
Ameeleza kuwa
amekaa eneo hilo tangu mwaka 1978 ambapo hivi sasa shamba lake limekuwa
likivamiwa na watu tofauti tofauti pasipo yeye kushirikishwa ikiwa
pamoja na kanisa kujengwa ndani ya shamba lake.
”Niliwahi
kuchimba msingi katika hili shamba ili nijenge alikuja mwenyekiti wa mtaa na
kuamuru ule msingi ufukiwe nisijenge hili eneo ni la kituo cha jamii (community
centre)”.
Pia mzee huyo
alisema ameshawahi kuandika barua kwa Mkurugenzi wa jiji kuwa sehemu yake ya
shamba ambayo haijatathiminiwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1999 ya ardhi.
”Mimi ni mkulima
wa shamba langu na sheria ile imeshapita kwa nini nisiipate ile sehemu yangu
ambayo kwa miaka 7 haikutathiminiwa kitu ambacho hakikutathiminiwa maana
yake hakihitajiki basi ningepewa mimi mwenyewe nitumie ikiwemo kujenga nyumba
yangu ya kudumu,” amesema mzee Kihendo.
0 comments:
Post a Comment