Takribani mwezi mmoja sasa tangu wachimbaji 15 wafukiwe na kifusi Nyarugusiu Wilayani Geita, balaa jingine la aina hiyo limetokea wilayani Butiama mkoani Mara, katika mgodi wa Buhemba ambapo watu 11 wameokolewa shimoni wakichimba dhahabu.
Kwa sasa wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Butiama kwa matibabu zaidi pia kazi ya uokoaji inaendelea kwa ajili ya kuwatafuta watu wengine ambao ndugu zao hawajawaona na wanahisi walikuwamo ndani ya shimo hilo amesema Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi.
Chanzo cha ajali hiyo ni mmomonyoko wa udongo uliosababisha kipande cha ardhi kuporomoka kutokana na mashimo kukaa muda mrefu richa ya kuwapo jua kali.
Nyamubi amesema mashimo hayo yaliachwa na mkoloni yako chini ya mwekezaji StanCom ambaye ndiye aliyekuwa akichimba dhanabu katika eneo hilo.
Kufuatia tukio hilo, viongozi mbalimbali walifika kushuhudia uokoaji akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara, DK. Charles Mlingwa.
0 comments:
Post a Comment