Katika chapisho la shirika
hilo kuhusu hatari ya kupata magonjwa hayo, WHO imesema kuwa magonjwa hayo kama
vile kiharusi, kisukari na saratani yanasababishwa kwa asilimia kubwa na
kudorora kwa miili kunakotokea katika nchi nyingi.
Kwa mujibu wa WHO, duniani
kote asilimia 81 ya watoto wanaopaswa kuwa shule hawafanyi shughuli za kufanya
viungo vya mwili vihusike na kuchangamka na badala yake wanabweteka.
Kazi hizo zinasaidia
kuboresha afya ya mwili na ni vyema zikafanyika mara kadhaa na kuepuka
kutofanya lolote kwa muda mwingi, limeshauri shirika hilo la afya ulimwenguni.
0 comments:
Post a Comment