Rais Adama Barrow wa Gambia |
Miongoni mwa wafungwa walioachiliwa huru hivi
karibuni nchini Gambia, ni miongoni mwa watakaounda baraza jipya la mawaziri
chini ya utawala wa raisi wa sasa Adama Barrow.
Amadou Sanneh alifungwa kwa tuhuma za
kuonekana ni mpinzani wa kisiasa wa kiongozi wa zamani Yahya Jammeh, katika
baraza jipya ameteuliwa kushika wadhifa wa waziri wa fedha saa sabini na mbili
mara baada tu ya kuachiliwa huru.
Mawaziri wengine tisa wamekwisha kula
kiapo chao, akiwemo waziri mpya wa mambo ya nje wa Gambia Ousainou Darboe, ambaye
naye alikuwa mpinzani mkubwa wa utawala wa bwana Jammeh, ambaye pia alishawahi
kufungwa na utawala uliopita.
Mawaziri wengine nane ambao bado
hawajajaza nafasi katika baraza la mawaziri, bado hawajafahamika.
Jammeh alikuwa mamlakani tangu mwaka
1994, aliondoka nchini Gambia na kuelekea uhamishoni mwezi uliopita, kufuatia
kushindwa kwa uchaguzi uliofanyika mwezi December mwaka wa jana na Adama Barrow
kuibuka mshindi.
0 comments:
Post a Comment