Friday 17 February 2017

SIMU ZA NOKIA 3310 KUREJEA…?

Kuna taarifa kwamba huenda simu muundo wa Nokia 3310 zikazinduliwa upya na kuanza kuuzwa tena baadaye mwezi huu.

Kampuni ya HMD Global Oy ya Finland, ambayo ina haki za kuunda bidhaa za nembo ya Nokia ndiyo inayodaiwa kuwa na mipango hiyo.
Simu hizo inaarifiwa zitazinduliwa wakati wa Kongamano la Simu za Rununu Duniani baadaye mwezi huu.
Kampuni ya Nokia ilinunuliwa na Microsoft mwaka 2013.
Simu asilia za Nokia 3310 zilipata umaarufu kutokana na uthabiti wake.
Nokia 3310/3330, zilizinduliwa 2000, na ni miongoni mwa simu zilizouzwa sana duniani. Jumla ya simu 126 milioni za aina hiyo zilitengenezwa na Nokia.
Una kumbukumbu za simu hiyo?
Dave Mitchell nchini Uingereza anaamini kwamba anamiliki moja ya simu za zamani zaidi aina ya Nokia 3310 nchini Uingereza.
Alinunua simu hiyo mwaka 2000 na anasema amekuwa akiitumia tangu wakati huo - bila natatizo yoyote.
Mwanajeshi huyo wa zamani anasema simu hiyo imewahi kufuliwa pamoja na nguo kwenye mashine, ikakanyagwa na hata kutumbukia kwenye mchuzi.
Anasema huwa inamhitaji kuweka chaji baada ya siku kumi.

Bado ina betri yake asili.

0 comments:

Post a Comment