Safari hiyo itafanyika 2018
kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SpaceX Elon Musk, alieongezea kwamba
watalii hao tayari wamelipa kiasi fulani cha fedha.
“Hatua hiyo inatoa fursa kwa binaadamu kurudi katika anga za juu
kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 45″alisema.
Wawili hao ambao majina yao hayakutajwa wataelekea mwezini
wakiwa katika meli hiyo ya angani ambayo itafanyiwa jaribio lake la kwanza la
kurusha rekoti isiokuwa na rubani.
Bwana Musk alisema kuwa ushirikiano wa shirika la sayansi na
teknolojia ya angani nchini Marekani Nasa umefanya ufanisi wa safari hiyo.
Amesema kuwa abiria hao wawili watasafirishwa kwa kasi zaidi ya
watu wengine wowote kuwahi kusafirishwa katika sayari.
Bwana Musk hatahivyo amekataa kuwataja abiria hao wawili
,akisema kwamba ni watu wanaojuana na kwamba hawatoki Hollywood.
Kama wanaanga wa Apollo, wawili hao watasaifiri angani wakibeba
matumaini na ndoto za binaadamu wote wanaopenda kusafiri.
Tunataraji kuwafanyia
ukaguzi wa kiafya kabla ya kuanza kuwafunza baadaye mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment