Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa
Rais Dkt. John Magufuli hajawahi kutangaza ama kutoa kauli ya kufutwa kwa vyama
vya siasa nchini.
Ametoa
kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi
ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe katika kipindi cha
maswali kwa Waziri Mkuu.
Katika swali lake Mheshimiwa Mbowe alisema Rais Dkt.Magufuli alinukuliwa
akisema atahakikisha anafuta vyama vyama vya upinzani na ifikapo mwaka 2020
hakuna upinzani nchini.
Pia Mheshimiwa
Mbowe alitaka kujua nini kauli ya Serikali kuhusu kunyimwa dhamana kwa Mbunge
wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema ambaye anashikiliwa kwa muda miezi
mitatu.
Mbali na
Mheshimiwa Lema pia kiongozi huyo alitaka kujua kuhusiana na kufungwa kwa
Mbunge wa Kilombelo, Mheshimiwa Peter Lijualikali pamoja na madiwani sita wa
chama hicho ambao wamefungwa na viongozi wengine 215 wanakabiliwa na kesi
mbalimbali.
“Kwanza nataka nikanushe kwamba Mheshimiwa Rais hajawahi kutangaza
kuvifuta vyama vya upinzani.Pia Watanzania wote wanajua nchi hii inaongozwa kwa
sheria, kanuni na taratibu i,” amesema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu
ameongeza kuwa “tunajua katika kuendesha nchi tunaendesha kwa mihimili mitatu
ipo Serikali, Mahakama na Bunge na hakuna mhimili unaoweza kuuingilia mhimili
mwingine,”.
“Pia Watanzania
wote wanajua kwamba jambo lolote ambalo lipo Mahakamani haliwezi kuzungumzwa
mahali pengine popote, hivyo siwezi kutumia nafasi hii kuzungumzia mambo yote
yanayoendelea chini ya sheria na yaliyo mahakamani,” amesema.
0 comments:
Post a Comment