Monday 6 February 2017

MTI MREFU ZAIDI AFRIKA WAGUNDULIWA TANZANIA…

Mti mrefu Afrika wagunduliwa katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania

Wanasayansi wanasema kuwa wamegundua kile wanaamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.

Wanasayansi kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti huo unaopatiknan karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani.
Mmoja wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita, lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu wake.
Mti huo kutoka familia ya Entandrophragma excelsum una urefu wa mita 81.
Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.

Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani

0 comments:

Post a Comment