Thursday 9 February 2017

HAYA NDIYO MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU RAIS MPYA WA SOMALIA..

Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohammed anaitwa jina la utani Farmajo aina ya chakula cha Kitaliano cha Jibini

Inasemekana kwamba alipenda sana kula Jibini wakati alipokuwa kijana wakati wa ukoloni wa Italiano.
Ana uraia wa nchi mbili za Marekani na Somalia na anajulikana kwa kampeni yake ya kupigania haki za kibinaadamu.
Amewahi kuhudumu kwa muda mfupi kama waziri mkuu mwaka 2011, lakini akajiuzulu baada ya miezi michache kufuatia migogoro kati yake na aliyekuwa rais Sheikh Sharrif hassa.
Hakuwa maarufu na wanasiasa wengine kwa kuwa alijionyesha kuwa mtu wa watu akipanda ndege za bei ya chini wakati alipokuwa akisafiri katika mataifa ya ughaibuni.

Miongoni mwa wagombea wote 20 ndiye aliyekuwa maarufu katika mtandao wa kijamii.

0 comments:

Post a Comment