Tuesday, 14 February 2017

AMUUA MFANYAKAZI AKIDHANI NI NGIRI AFRIKA KUSINI..

Watu nchini Afrika Kusini wamegadhabishwa, kufuatia taarifa za mwanamme mmoja, ambaye analaumiwa kwa kumuua kwa kumpiga risasi mfanyakazi wa shamba, akidhani kuwa mtu huyo ni ngiri.

Stephen Hepburn alifikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka ya mauaji.
Yeye na mwenzake wa kike walikuwa wakiwawinda ngiri kwenye shamba moja lililo mkoa wa Limpopo kaskazini siku ya Jumamosi, wakati Jan Railo ambaye alikuwa na umri wa miaka 23 aliuawa.
Msemaji wa Polisi Motlafela Mojapelo aliiambia BBC kuwa Bwana Hepbaun, alikamatwa siku ya Jumatutu.
Mojapelo aliongeza kusema kuwa bwana Hepburn alisema kuwa aliafyatua risasi eneo ambapo alisikia sauti alipokuwa akiwinda, na alipoenda kuangalia akapata kuwa ni mtu alikuwa amelala chini.

Wanachama wa tawi la chama cha ANC eneo hilo ambao waliofika mahakamani walisema hawaamini ikiwa mauaji hayo yalikuwa ya kimakosa.

Related Posts:

  • MKUU MPYA WA FBI APATIKANA…… Bunge la Seneti nchini Marekani limepiga kura ya kuthibitishwa Bwana Christopher Wray kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani la FBI. Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu James Comey alipotimuliwa na Rais Dona… Read More
  • RAIS MUSEVENI: SIJAUGUWA KWA MIAKA 31 Mara nyingi kumekuwa na ripoti za kuugua kwa marais, hasa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Bwana Buhari amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa ambao haujulikani mjini London tangu mwezi Mei, ambayo ni ziara ya pili anafan… Read More
  • KAMPUNI YA CHINA YASHTAKIWA KWA KUCHAFUA MAZINGIRA GAMBIA….. Wanamazingira kutoka miji midogo ya pwani nchini Gambia wameipeleka kampuni moja ya China mahakamani kwa madai ya kutupa takataka za sumu kwenye bahari. Hatua hiyo inakuja baada ya serikali kukubaliana nje ya mahakama n… Read More
  • MWIZI AKUTWA AMELEWA NDANI YA NYUMBA ALIOVUNJA…. Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia kwa wizi, baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani. Polisi wanasema jamaa huyo wa miaka 36 alivunja na ku… Read More
  • BIBI HARUSI AJARIBU KUMUUA MUMEWE BAADA YA NDOA Bibi harusi katika jimbo la Tennessee nchini Marekani, ametiwa nguvuni baada ya polisi kusema kuwa alitoa bunduki kwenye gauni lake la harusi na kumtishia mumewe saa chache tu baada ya kufunga ndoa. Kate Elizabeth Prich… Read More

0 comments:

Post a Comment