Tuesday, 7 February 2017

WATUHUMIWA DAWA ZA KULEVYA WAFIKISHWA MAHAKAMANI..

Takriban watuhumiwa 10 wa dawa za kulevya ambao ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi hii.


Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani sasa ni wasanii Rommy Jones, TID, Babuu wa Kitaa, Petit Man, Tunda (model wa kike), Lulu Diva, Recho, Joan, na wengine.

Watuhumiwa wote wamesomewa kiapo cha Mahakama ambapo pande wa Jamuhuri umeomba watuhumiwa hao waamrishwe kuwekwa chini ya uangalizi kwa kuripoti polisi mara 2 kwa mwezi kwa kipindi cha miaka 2 ili kuangaliwa kama wameacha tabia ya kutumia dawa hizo hususani bangi
                      
Wakili wa upande wa utetezi amedai taarifa hizo hazijakamilika, kwani hazioneshi wanaojiusisha na dawa za kulevya na walikamatwa lini na wapi.


Pia amesema hakuna ushahidi wa kujitosheleza wa madai hayo kiasi cha wao kupata dhamana ya kuangaliwa tabia zao bila polisi kutoa ufafanuzi wa kina wa kwanini wanahitaji kupata dhamana ya uangalizi wa nidhamu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment