Tuesday 28 February 2017

VYOMBO VYA PLASTIKI CHANZO CHA SARATANI….

Imebainika kuwa vifaa vya plastiki hutengenezwa kwa kemikali zaidi ya 200, hivyo kuwa chanzo cha aina 100 za ugonjwa wa saratani.

Vifaa hivyo vya plastiki ni pamoja na mifuko ya rambo, bakuli, vikombe na vifaa vya kuhifadhia chakula (makontena).
Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Marafiki wa Watoto wenye Saratani Tanzania Walter Miya, wakati wa uhamasishaji wa kupima afya kwa watoto.
Amesema toka matumizi ya plastiki yazidi kuongezeka nchini, ugonjwa wa saratani nao umeongezeka, hasa kwa upande wa akina mama.
Ugonjwa wa saratani umekuwa ukiharibu ukuaji wa mfumo wa uzazi hususani kwa watoto ambao bado kuzaliwa, mabadiliko ya kijenetiki na kushindwa kuona vizuri.
Amesema kupitia utafiti mdogo walioufanya, inaonyesha asilimia 60 za saratani zimesababishwa na matumizi ya vifaa vya plastiki.
Amesema jamii inapaswa kupunguza matumizi ya vifaa vya plastiki, kutokana na madhara yaliyomo katika vifaa hivyo.
Hata hivyo amesema wanahitaji sera na sheria dhidi ya matumizi ya plastiki, kutokana na kukithiri kwa vifaa hivyo ambavyo vimekuwa vikitengenezwa kila kukicha viwandani.

0 comments:

Post a Comment