Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imepandisha bei za mafuta ya
aina zote kuanzia leo isipokuwa Mkoa wa Tanga pekee.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Felix Ngalamgosi, jijini Dar es salaam
alipokuwa akizungumza kuhusu kupanda kwa bei za mafuta ya jumla na reja reja
kwa mafuta ya aina zote.
“Kwa
Februari 2017,bei za reja reja zimepanda, petroli imepanda kwa shilingi 69 kwa
lita sawa na asilimia 3.64 ambayo ni shil. 1,959, dizeli ni shil.129 kwa lita
ambayo ni sawa na asilimia 7.47 ambayo ni sh. 18,61 na mafuta ya taa ni sh.151
kwa lita, sawa na asilimia 8.90,ambayo ni sh.1,852, kwa mkoa wa Dar es
salaam,” amesema Ngalamgosi.
Amesema
kuwa kulingana na toleo la Januari bei za jumla nazo zimepanda ambapo petroli
ni sh.69 kwa lita sawa na asilimia 3.86,dizeli sh.129 kwa lita ambayo ni sawa
na asilimia 7.96 na mafuta ya taa ni sh.151 kwa lita sawa na asilimia 9.50.
Amesema
kuwa kupanda kwa bei ya mafuta kunatokana na mabadiliko ya bei za mafuta kwenye
soko la dunia,kuongezeka kwa gharama za usafirishaji na kushuka kwa thamani ya
shilingi dhidi ya dola ya Marekani.
Hata
hivyo amesema kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya bei za mafuta kwa Mkoa wa
Tanga,kutokana na kutopokea mzigo mpya wa mafuta kwenye bandari ya Tanga kwa
mwezi Januari.
0 comments:
Post a Comment