Mahakama ya Juu nchini India imefuta
leseni za madaktari 634 ambao wamejipata kwenye sakata ya wanafunzi kutumia
udanganyifu kujiunga na vyuo vya mafunzo ya udaktari katika jimbo la Madhya
Pradesh.
Mamia
ya wanafunzi, imebainika, walitumia udanganyifu kujiunga na vyuo vya mafunzo ua
udaktari kati ya 2008 na 2013.
Maelfu
ya watu wamekamatwa kuhusiana na kashfa hiyo ambayo imepewa jina Vyapam
Vyapam
ni ufupisho wa afisi ya serikali ambayo husimamia mitihani kabla ya watu kupewa
kazi za serikali au kujiunga na vyuo majimbo nchini India.
Kwenye
uamuzi wake, Mahakama ya Juu imesema waliofutiwa leseni walijihusisha katika
"vitendo vya udanganyifu" na "ulaghai wa kiwango kikubwa".
Kashfa hiyo
ilihusisha kuvujishwa kwa karatasi za mitihani, kudanganya kupitia karatasi za
majibu ya mitihani na pia kukodishwa kwa wanafunzi werevu kufanyia mitihani
watahiniwa wengine.
Kadhalika,
nafasi za kuingia vyuoni viliuziwa watu walioweza kulipa pesa nyingi.
Waandishi wa habari
wanasema nafasi moja chuoni iligharimu kati ya rupia 1 milioni ($15,764;
£10,168) na rupia 7m.
Watu
zaidi ya 2,000 wametuhumiwa kuhusika katika kashfa hiyo tangu 2012.
Watu
33, wengi wao wakiwa watuhumiwa katika kashfa hiyo, wamefariki katika hali ya
kutatanisha katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
0 comments:
Post a Comment