Hospitali moja nchini Uchina imekiri
kwamba watu watano waliambukizwa virusi vinavyosababisha Ukimwi hospitalini
humo kimakosa.
Waliambukizwa
na mhudumu wa afya ambaye alitumia tena vifaa vya matibabu ambavyo vilifaa
kutupwa baada ya kutumiwa.
Maafisa
wanasema mhudumu huyo alitumia bomba lililotumiwa kumtibu mgonjwa mwenye Ukimwi
kwa wagonjwa wengine.
Maafisa
wa utawala wa mkoa wametaja kisa hicho kama "ukiukaji mkubwa wa
utaratibu".
Tayari
wahudumu watano wamefutwa kazi katika hospitali hiyo ya mkoa ya Zhejiang katika
mkoa wa Hangzhou.
Maafisa hao wa afya
wa mkoa wamesema walifahamishwa kuhusu kisa hicho 26 Januari.
Lakini
kwenye taarifa, hawajasema iwapo kuna wagonjwa wengine ambao huenda waliwekwa
kwenye hatari ya kuambukizwa na ni maradhi ya aina gani wale walioambukizwa
walikuwa wakitibiwa.
Wale
walioambukizwa watapokea matibabu na fidia, taarifa fupi ilisema.
Katika
ripoti ya hivi karibuni, China ilisema kulikuwa na watu 501,000 waliokuwa
wameambukizwa virusi vya Ukimwi kufikia mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment