Mawasiliano ya simu kati ya Rais wa Marekania Donald Trump na waziri mkuu
wa Australia Malcolm Turnbull, yamezua maswali kuhusu makubaliano ya kuwachukua
wakimbizi.
Gazeti la Washington Post
liliripoti kuwa bwana Trump alitaja mawasiliano hayo kuwa mabaya zaidi kati ya
yale aliyoyafanya na viongozi wa dunia siku hiyo, ambapo aliikata simu hiyo.
Bwana Trump kisha
aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa atafanyaia uchunguzi makubaliano hayo.
Makubaliano hayo
yaliyoafikiwa wakati wa utawala wa Rais Obama, yatasababisha hadi watafuta
hifadhi 1,250 wanaoelekea Australia kupewa hifadhi nchini Marekani.
Australia imekataa
kuwakubali wakimbizi wengi wao wakiwa ni wanaume kutoka Iran, Afghanistan na
Iraq na badala yake wamewazuilia katika vituo vilivyvo kwenye visiwa vya Nauru
na Papua New Guinea.
Waziri mkuu Turnbull
amekuwa akitaka kujua hatma ya makubaliano hayo baada ya Trump kusaini amri ya
kuzuiwa kwa muda wakimbizi kutoka nchi saba zilizo na waislamu wengi kuingia
nchini Marekani.
Bwana Turnbull baadaye
alsema kuwa alikasirishwa kuwa mawasiliano hayo yaliwekwa hadharani.
Alikiambia kituo
kimoja cha redio mjini Sydney kuwa ripoti kwamba Trump alikata simu si za
ukweli
0 comments:
Post a Comment