Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema mapambano dhidi ya vita ya biashara ya madawa ya kulevya si ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda peke yake,
ni vita ya watanzania wote, hivyo ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi, na wengine wanaohusika kushikamana na kupambana na biashara hiyo haramu bila kujali umaarufu wa mtu, wala cheo chake.
Rais Magufuli amesema hakuna asiyejua madhara ya madawa ya kulevya, madhara hayo kwa taifa kwa taifa letu yamefikia mahali pabaya, ‘haiwezekani watu wanauza kama njugu’ Amesema Rais Magufuli