Thursday, 9 February 2017

WAFUASI 11 WA AL-QAEDA WAUAWA, YUPO MSHIRIKA WA OSAMA..

Wizara ya ulinzi nchini Marekani imesema Wanajeshi wa nchi hiyo wamewaua takribani wafuasi 11 wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda kupitia mashambulio mawili ya kutoka angani karibu na mji wa Idlib nchini Syria mwezi huu.

Taarifa hiyo iliyotolewa na msemaji katika wizara hiyo, Kapteni Jeff Davis imeeleza kuwa kati ya wapiganaji hao waliouliwa ni mshirika mkuu wa zamani wa aliyekuwa kiongozi wa Al-Qaeda, Osama Bin Laden huku wengine 10 wakiuawa kwenye shambulio moja Februari 3.
Amesema shambulio la pili tarehe 4 Februari lilimuua Abu Hani al-Masri, aliyekuwa na ushirika wa karibu sana na Osama Bin Laden.
Pia kwa mujibu wa taarifa hizo, Al-Masri inadaiwa kuanzisha na kuendesha kambi za mafunzo za al-Qaeda nchini Afghanistan miaka ya 1980 na 1990.

“Mashambulio haya yanavuruga uwezo wa al-Qaeda kupanga na kutekeleza mashambulio ya moja kwa moja ya kulenga Marekani na maslahi yake kote duniani,” amesema Kapteni Davis.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment