Friday, 3 February 2017

JPM AFANYA UTEUZI WA MKUU WA MAJESHI…

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.
Aidha, Jenerali Venance S. Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali James M. Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.
Luteni Jenerali James M. Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa hapo baadaye.

Related Posts:

  • WANAOTOA SIRI ZA SERIKALI MTANDAONI KUTUPWA JELA MIAKA 20.. Serikali imetoa onyo kwa watumishi wa umma wanaotoa siri za serikali na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa watachukuliwa hatua za kisheria. Onyo hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Ofisi ya R… Read More
  • NYAMA IKAE SAA NANE KABLA YA KUPIKWA............. Nyama nyekundu ni kitoweo kitokanacho na wanyama. Mbali na wanyama wa porini, watu wengi hupata nyama hiyo kutokana na kuchinja wanyama wafugawao kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na ngamia. Nyama nyekundu hutakiwa kuandaliwa… Read More
  • MKAPA MIONGONI MWA WAATHIRIWA WA UPANUZI WA BARABARA... Nyumba inayoaminika kumilikiwa na mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Tanzania Benjamini Mkapa itavunjwa ili kuruhusu upanuzi wa barabara ya Morogoro. Nyumba hiuyo ya Anne Mkapa itakuwa miongoni mwa maelfu ya nyumba, a… Read More
  • TUNDU LISSU ATEMA CHECHE…. Wakati Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, akiwa bado anakabiliwa na kesi kadhaa za uchochezi, amefytuka tena na kutoa maneno mazito juu ya viongozi wa Serikali, huku akisema kwa … Read More
  • AMUUA MUMEWE KISA AMEWAHI KUINGIA BAFUNI... Mgini Aron 37 mkazi wa Magunga Wilaya ya Butiama Mkoani Mara, amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mkewe Jeni Mwenda 25, kwa sababu ya wivu wa mapenzi. Akizungumza na waandishi wa habari ofisin… Read More

0 comments:

Post a Comment