Wednesday 25 April 2012

KWA NINI VIUMBE WENGI WANA MACHO MAWILI

Nilikuwa natafakari juu ya uumbaji na kushangazwa na kitu kimoja cha ajabu; viumbe vingi hata vinavyoishi mazingira tofauti na vya aina (specie) tofauti sana vimefanana kwa kuwa na macho.


Vinaweza vyote visiwe na miguu, mbawa, au pua lakini karibu vyote vina macho. Kuanzia majini, angani na nchi kavu viumbe vingi vinamacho! Wadudu wadogo na wanyama wakubwa wote wana macho; samaki na ndege hadi minyoo ina macho! 

Na katika maajabu ndani ya maajabu ni kuwa viumbe vingi vina macho mawili (sijajua kama yupo mwenye jicho moja) na vile vingine vina macho mengi (compound eyes). Angalia mifano hii:

Angalia Nyoka:




Angalia Samaki:




Angalia Ndege:


Angalia Vipepeo


 


Angalia Mchwa





Angalia Nyangumi


Angalia Kaa:



Angali Nyani:




Kwanini?
Jibu la kisayansi ambalo hutolewa mara nyingi ni "evolution"; lakini kwanini "eyes"? Utaona viumbe vinafanana vitu vingi tu lakini mara nyingi tofauti ni idadi.


kwa mfano viumbe vingi vina miguu minne (wanyama) lakini vipo vyenye miguu sita (wadudu) na vingine havina miguu kabisa (nyoka na samaki); lakini vyote vina macho! Kwanini macho ni mojawapo ya viungo ambavyo vinaonekana karibu katika viumbe vingi zaidi kuliko viungo vingine? Na kwanini mara karibu zote macho hayo yanakuwa mawili siyo matatu au manne (kuangalia pembeni, juu na chini)? 

0 comments:

Post a Comment