Tuesday 17 April 2012

Washindi wa tuzo za Kili Music Awards Tanzania 2012






Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utuzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora za Kilimanjaro Music Award 2012 zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania  na nje ya nchi, Diamond amejipatia tuzo tatu kwa mpigo.


Diamond ambaye mwaka 2010 aliibuka pia kidedea kwa kuzoa tuzo nyingi na mwaka 2011 kumpa nafasi 20% kwa kuzoa tuzo nyingi mwaka huu amenyakua tuzo ya MTUNZI BORA WA MWAKA, MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME na vyake ya Mawazo ikinyakua tuzo ya VIDEO BORA YA MWAKA (video inaonekana hapo juu).

Mbali na Diamond aliyebahatika kunyakua Tuzo mbili katika tuzo hizo ni msanii mwingine wa Bongo Fleva Suma Lee aliyenyakua tuzo za WIMBO BORA WA AFRO POP ambao alipata kupitia wimbo wa HAKUNAGA na Tuzo ya pili ni ya WIMBO BORA WA MWAKA ambao pia ni HAKUNAGA.

Aidha msanii Chipukizi wa Bongo Fleva, Omy Dimpoz naye ametamba baada ya kunyakua tuzo ya WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA wa  NAI NAI aliomshirikisha ALI KIBA na pia alitwaa tuzo ya MSANII BORA ANAECHIPUKIA kupitia wimbo wake huo huo wa NAI NAI.

Roma Mkatoliki a.k.a Mpare wa Milimani alikuwa katika kundi hilo la wasanii wenye tuzo mbili baada ya kupata tuzo ya WIMBO BORA WA HIP HOP wa  MATHEMATICS (bofya hapa kuzikiliza) na Tuzo ya MSANII BORA WA HIP HOP.

Wasanii na Vikundi vingine ambavyo vilijinyakulia tuzo ni pamoja na  WIMBO BORA WA RAGGAE Ulikuwa ni ARUSHA GOLD wa kundi la WARRIORS FROM EAST huku Tuzo ya WIMBO BORA WA DANCE HALL ukiwa ni MANENO MANENO wa QUEEN DARLIN.

Tuzo ya WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA alienda kwa Ali Kiba kupitia wimbo wake maarufu wa DUSHELELE, Tuzo ya WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI ilikwenda kwa A.T kwa kibao cha VIFUU UTUNDU.

Tunzo nyingine ilikuwa ni ya  WIMBO BORA WA TAARABU aliyonyakua mwana dada wa kikurya anaeimba Taarabu Aisha Mashauzi kupitia wimbo wa NANI KAMA MAMA wa kundi lake la Mashauzi Classic.

Kundi la Twanga Pepeta nalo lilijinyakulia Tuzo ya WIMBO BORA WA KISWAHILI kupitia wimbo wa DUNIA DARAJA huku Tuzo ya WIMBO BORA WA R&B ikienda kwa Ben Paul kwa wimbo wa NUMBER ONE FAN. 

Tuzo nyingine katika mfululizo huo wa Kili Music Award 2012 ilikwenda kwakalijo Kitokololo aliyepata Tuzo ya RAPA BORA WA BAND ambapo Tuzo ya WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI ilienda kwa Wimbo wa KIGEUGEU uliyoimbwa nae JAGUAR.

Tuzo zingine ni za MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE iliyoenda kwa KHADIJA KOPA, tuzo ya  MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI ilienda kwa MANEKE.

Tuzo ya HALL OF FAME ilienda kwa TAASISI JKT, Tuzo ya HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI ilienda kwa Mtu mzima KING KIKII na HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI Ilinyakuliwa na Hayati REMMY ONGALA.

Mkonngwe wa uimbaji wa nyimbo za Kibongo Judith Wambura Habash "Lady Jay Dee' alinyakua tuzo ya ya MWIMBAJI BORA WA KIKE huku kijana aliyeshika kasi kutoka kundi la THT Barnaba akifunga jahazi hilo kwa kunyakua tuzo ya MWIMBAJI BORA WA KIUME.

0 comments:

Post a Comment