Wednesday 18 April 2012

Uvutaji wa sigara katika ndoa:





Wake au waume wa wanandoa ambao wanavuta sigara wamekuwa na wakati mgumu sana katika hisia zao,hasa kutokana na tabia ya kuvuta sigara kwa hao partners wao.

Hisia huweza kuwa ni za hofu, mashaka na kujisikia kutothaminiwa au kuwa disappointed na hata kuumizwa na hiyo tabia.



Wapo partners ambao hutafsiri kwamba kitendo cha kutoacha kuvuta sigara,ni kuonesha kutojali afya yake mvutaji na familia kwa ujumla yaani mke, mume na watoto.


Anyway kila mvutaji hupenda kuacha kuvuta sigara hata hivyo hamu na uhitaji wa kuvuta sigara huwa kubwa zaidi,kuliko makali ya kifo hii ina maana mvuta sigara akiwa na hamu ya sigara huwa radhi kukubali kuvuta sigara kuliko kutovuta kwa kuogopa kifo.


Ukishajiingiza kwenye kuvuta sigara na kuwa addicted na nicotine iliyomo katika Sigara,utakuwa radhi kukubali kifo kuliko kuacha kuvuta.


Kumbuka:

Wavuta sigara huwa na magonjwa mengi kuliko wasiovuta,pia wavuta sigara huishi muda mfupi kuliko wasiovuta.

Ukivuta sigara kwa zaidi ya miaka 30 unaweza kuwa umetumia pesa yenye thamani ya zaidi ya TSh. millioni 200.



By Kiwa strong


0 comments:

Post a Comment