This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday, 21 August 2012

BARUA KWA VIVIAN TILLYA FROM teamSUA-HIP HOP Dear Vivi....


Ni miaka saba sasa tangu uondoke na tunakukumbuka sana michano yako na mambo mengine mengi....(jalini ubinadamu msifanye mavitu kama sanamu.....). Natumai umeonana na Faza Nelly,DOG Nacko.Papaa,Mlost na Pacha Izzy na wengine wengi waliokuja huko.

Dhumuni la barua hii ni kukusalimu na kukujulisha yanayoendelea Arusha.
Mengi yametokea ila ya Muhimu kukufahamisha kuhusu harakati za Muziki hapa Arusha.
Imagine eti siku hizi Metropole,Ricks,Mawingu na Crystal club hazipo tena.
Machizi wengi wamehamia Dar es salaam(just like you...) ila wao wamebadilisha hadi majina wanakuja Arusha kufanya show na kusepaz.
Machalii wapya kibao kwenye Game na wanakalisha usipime wengine wako mbele na wanafanya harakati zilezile Kzz wa X plastaz hajarudi bado tangu aende na anatoa Mixtape moja kali sana hivi karibuni,Chindo pia anawakilisha akiwa huko si unajua tena Jamaa alivyo mbishi.
Jcb na Spark bado ni hardcore(...wana makid asee).

maprodyuza wengi wapya na Studio nyingi.WATENGWA kuna Daz Naledge,DX amekuja na Noizmeka,hata Ngalimi siku izi kuna Studio asee KZ kaja na KAZAWAZA.Grandmaster siku izi wanapiga mpaka VIDEO bana.zipo mingi siwez hata kuzitaja zote.

Harakati zote zile za rap sasa hivi zimeamia Kijenge ya Juu(S.U.A Free-Stage

Watu kibao wanakutana na kupiga freestyle,michano na magrafiit kibao.

Si unakumbuka vile ulikua ukikasirika kuona hakuna mademu kwenye HIPHOP concert na ukawa unaamua kuonyesha uwezo wako dah! ulikua unakalisha asee(.....sa nani wakuongoza safari wote tunaujua usukani.......siwaelewi! )
Juzi si kuna madem wakaibuka SUA bana asee tulikukumbuka sana laiti ungekuwepo ungefarijika kinyama.

Kuna redio stesheni mingi niaje! karibu kila mtaa na maclub za kutosha huko town usiku kama tu mchana. ... kuna masista Dread wengi peace kama wewe.... inapendeza

Arif mambo kibao yamebadilika... kutoka TAPE na disc man siku izi kuna mavitu yanaitwa I-pod,I phone na ma-I pad kitu touch screen maamaaa si unajua Swagga tena...(sorry i know you now know about Apples kama sio matunda tena nikikuambia mambo ya Blackberry si ndo utadata kabisa...hahahahaha!!)

I will tell you about it next time sahivi naenda misele so kama vipi mpe hi Complex(Mwambie alivyosepa tu BTOWN CLAN wakaNYAMAZA ooh SH**T MIKOSI WAMENYAMAZA.....),James Dandu,Drob,Steve2k,produza Roy na wengine mlioko nao huko.

Jumapili tarehe 26 SUA itakua ni spesho kwako na Complex wa2 watapiga mistari yenu..oooyyyy! .Nitakujulisha zaidi next time.

Wako Wapendwa
Katika HIP HOP
###teamSUA###


VIVIAN TILYA  ALIFARIKI DUNIA 21AUGUST KWA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MBWEWE AKIWA NA COMPLEX.

UNAKUMBUKWA NA FAMILIA YAKO NDUGU JAMAA NA MARAFIKI.

NAAMINI UMEKUTANA  NA FREDY JEBI, FATHER NELLY, MLOST NA PACHA ONE.

TUTAZIDI KUWAKUMBUKA..BWANA ALITOA NA BWANA ALITWA UPUMZIKE KWA AMANI VIVIAN.
AMENI.........Saturday, 11 August 2012

Exclusive: Makala ya kusisimua kuhusiana na maisha magumu ya mdogo wake ObamaObama's slumdog brother: Kutana na mlevi asiye na matumaini aishie jijini Nairobi ambaye ni mdogo wake na rais wa Marekani


Makala hii imetafsiriwa kutoka kwenye gazeti la Daily Mail mwandishi akiwa  ANDREW MALONE. Makala hii imechapishwa jana, August 10, 2012.

Wakati mwanaume mrefu na anayejulikana sana akiondoka kwenye kibanda chake kilichopo kwenye makazi fukara kabisa barani Afrika wiki hii, baadhi ya watu walianza kumuita kwa utani:‘Mister President! Mister President!’

Akielekea kupata kifungua kinywa huku akivuka mifereji inayotiririsha maji machafu, muonekano wa jamaa huyu mrefu na aliyekonda, unavutia vicheko vya chini chini kutoka kwa watoto wanaocheza kwenye jalala.

              George akiwa kwenye nyumba anayoishi

Jina la jamaa huyu ni George Hussein Obama, ni mdogo wake na Barack Hussein Obama, rais wa kwanza mweusi wa Marekani na mwanaume anayeheshimika zaidi duniani.

Wanaume hawa wawili wanachangia baba lakini Barack Obama alizaliwa Hawaii kwa mke wa pili wa baba yao ambaye ni mmarekani na George alizaliwa nchini Kenya akiwa mtoto wa mke wanne wa mzee huyo.

Leo, wakati Barack akifurahia maisha kwenye Ikulu ya White House, akiruka kwenda nje na Air Force One na ni rafiki wa mastaa wa filamu na wengine mashuhuri, George, 30, anapatikana akiwa amechoka kwenye makazi yake ambayo hata wakazi wenzake wa eneo hilo maskini jijini Nairobi wanayaona kama kichuguu.
Ingawa anadai kutotumia heroin au cocaine, George hutumia muda mwingi kunywa Gongo (Chang’aa) kuanzia anapoamka mpaka muda ambao huanguka na kuzima kabisa.

Gongo anayokunywa ni ile iliyochanganywa na kemikali ya ethanol, na kuongezea acid kutoka kwenye betri ili kuipa kick zaidi, na mchanganyiko huu husababisha upofu na kifo inapochanganywa vibaya.

Kiasi kidogo tu cha pombe hiyo huwafanya hata wanywaji wazoefu kulewa kiasi cha kushindwa hata kukumbuka majina yao. Wanywaji wa mara kwa mara huathrika maini na figo ama ubongo.


Nilipomtafuta George asubuhi siku moja kufahamu maisha yake, alikuwa tayari kwenye kibanda kimoja jirani akinywa Chang’aa ambapo ngono na machangudoa ni sehemu ya menu na hufanyika kwenye kitanda kilichowekwa nyuma.

Utambulisho unafanywa na ‘mpambe’ wa George  — mkazi wa eneo hilo mwenye macho mekundu na mnywaji mwenzie ambaye anamvuta George nje ya kibanda hicho na kumwabia aje kumuona mzungu nje (shouting at him to come and see the ‘muzungu’ (white man) outside.

Baadaye baada ya kusalimia, ninafanya kosa. Namkaribisha George kwaajili ya chakula cha mchana kwenye hoteli yangu. Kwa siku mbili zilizofuatia, aliivamia baa yangu ndogo, kuwaalika wapenzi wake kibao na washkaji zake kula na kunywa kwa gharama zangu na kujionesha kama staa aliyeharibikiwa.

Aliomba pia ‘kitu kidogo’ — Swahili for something small, which, of course, means something large and financial — na alichukia baada ya mimi kukataa kuwapa hela mademu zake.

George pia aliendelea kulaumu kuhusu jina la Obama kuwa kama mzigo na laana kwake, ilhali wakati mwingine bila aibu hulitumia jina hilo kupata hela nyingi iwezekanavyo ili kuzitumia kunywa na kuvuta bangi.

‘Watu wanavutiwa na mimi kwasababu ya kaka yangu,’ anashusha pumzi na kushusha  Johnnie Walker mbili kwa mpigo. ‘Nachukia’. Watu wanapenda niwe mtu mwingine.’

Mara ya kwanza George alikutana na kaka yake alipokuwa shule ya msingi. Barack alienda Nairobi miake michache tu baada ya baba yao kufariki kwa ajali ya gari. George anakumbuka alikuwa akicheza soka wakati kaka yake alipowasili kumsalimia.

Mara ya pili wanakutana ni kipindi Obama — alipokuwa Senator na alifanya ziara ya Afrika Mashariki mwaka 2006, na kutembelea Nairobi kuiona familia yake.


George anasema kwa sasa watu wanamshinikiza afuate nyayo za kaka yake kwenye siasa. ‘Nina watu wengi ambao huniambia nigombee ubunge. Lakini sivutiwi na siasa.’

Kisha anatulia, na kuongeza: ‘Lakini kama Barack angekuwa rais na mimi ningekuwa rais wa Kenya ingekuwa rahisi kuonana.’

Anasema umaskini wake ndio unawazuia ndugu hao kuwa na uhusiano wa karibu.


‘Ana majukumu. Hatakiwi kunilea mimi,’ anasema. Mimi ni mtu mzima, kila mtu hudhani kuwa huwa ananitumia fedha. Lakini mimi sio ombaomba.’ Lakini alipoulizwa iwapo aatachukua fedha akipewa na Obama alisema: ‘Seriously! Yes! Who wouldn’t?’

George alikulia jijini Nairobi akiwa na mama yake ambaye aliolewa tena na mfaransa aliyekuwa anafanya kazi kwenye shirika la misaada jambo ambalo anadai lilimfanya awe hivyo.

Alianza kunywa pombe na kuvuta bangi akiwa na miaka kumi, miaka mitano baadaye alifukuzwa kwenye shule ya boarding, ambako alicheza rugby na kujifunza lugha za kigeni kutokana na kutumia madawa ya kulevya.

Anakubali kuwa alikuja kuwa addicted na cocaine na heroin akiwa na miaka 17, na kuwa mwizi wa kutumia silaha ili kupata hela ya kunywea pombe.

Mwaka 2003 alifungwa jela kwa kosa la kuiba kwa kutumia silaha.

Alikaa kwa miezi tisa kabla ya kutoka kutokana na kukosekana ushahidi.

Swali ni je! George anastahili kuishi maisha haya wakati kaka yake ni rais wa Marekani?

Friday, 10 August 2012

LINEX AOMBA RADHI WANAWAKE WOTE NA JAMII KWA UJUMLA

siku chache baada ya msanii Linex kutoa video ya wimbo wake (AIFOLA), ameandika katika ukurasa wake wa facebook, akiomba radhi kwa wanawake wote kutokana na kipande cha video yake ikimuanyesha akimpiga kofi mschana aliekuwa anaigiza nae katika video hiyo kutokana na kupata malalamiko mengi yanayodai kuichochoa jamii katika vitendo hivyo hasa kwa wanaume

"Naomba radhi kwa kila mwanamke Dunian kofi nililompiga vdeo gal wa kwenye aifola vdeo sikua nakusudia uchochezi wa mwanamke kupigwa na mwanaume wake natumai wanaume wenzangu mmenielewa lengo ilikua kutafuta uhalisia wa matukio kwenye vdeo yangu #team mwanamke hapigwi analiwazwa na kubembelezwa..." amesema linex
KUTOKA KWENYE MUZIKI HADI TV,DRAMA INAYOITWA FXDr.Dre ni kati ya wasanii wa Hip Hop waliopata heshima sana katika game na alitajwa katika marapper watano wenye mkwanja akiwemo P.Diddy, Jay Z, Birdman, 50 cent na yeye mwenyewe Dr Dre. Katika mauzo ya headphones zinazofahamika kama beats by dre zilimumrudisha Dre hadi juu na kuwa kati ya marapper wenye mkwanja, Na kwa sasa yuko tayari kuanza kuonekana kwenye Tv Drama mpaka sasa bado anaendelea kumalizia script ya Drama FX.

SINTA:HUYU NI NANI?ETI MUIMBAJI?HAPATIKANI HATA GOOGLE AU NDIO WALE KIINGILIO BUKU UZINDUZI TANDALE

leo hii katika pita pita zangu, nimekutana na story hii iliyoandikwa kupitia sintah.com, ikionekana kuwa ni majibu kwa Ney wa mitego, baada ya kuongea kwenye Take one kuhusu single yake ya NASEMA NAO na kumtaja mwanadashosti Sintah kuwa anafanya chochote kile ilimradi arudi kwenye game...... na haya ndio majibu yaliyofumuka.....
hivi wa wapi weweee,mbona husomeki weweee,tume google
hupatikani wewe,shukurani kwa mdogo wako alietuletea picha yako ya beach, sijui nani sijui nay utaweza??
jipange,namuonea huruma mama yako kuzaa kiumbe
kilichoharibikiwa, nina jaribu ku google naona neyo wa Us sasa nisaidie nitupie kwa mnyamani au kiembe mbuzi niambieeee ili nikupate my brodaaaaa you have just tickled a private part of a tiger,,, you wanted promo now you gotta maza vitumbua 
NEY WA KUJITEGA MWENYEWE MAANA
UNA CHASTE  MBU SIJUI UTAMTEGA NANI, KAMA UNA SHIDA NA MIMI DJ DJ DJ AND MY BRODAA CHOKA ANAJUA NINAPOEGESHA MILONJO YANGU  SASA KAMA UNATAKA KUIKATA KAMA ULIVYOWAMBIA WATU WAKO BBM(MAANA HU HUNA HADHI YA KUKAA KTK MY BBM LIST) MWAMBIE AKULETE MDOMO HUPONZA KICHWA NA UMEJIPONZA LOVES LEO NIMEWAFUNGULIA COMMENT MTU AKIGUSWA ATAJIJUA MAANA NIMECHOKA KUONEA WATU HURUMA KAMA NOMA NA IWE NOMA
NEY NIMESHAMPA RUHUSA MLINZI AKURUHUSU UINGIE SWALI ANAKUJUA??? JIPANGE ULIPOCHOKOZA SIPO KABISA UNSTOPPABLE NOTHING BUT CONFIDENCE
MSICHANA AMBAYE ANA TWO SIDES (COOPERATE FIGURE NA ACTRESS) OOH SORRY USIJE MCHANA NITAKUWA SERENA NINA APPOINTMENT NA WORLD BANK CREW CONCERNING MY LAUNCH  

SINA SHIDA NA  MTU ILA UKINIANZA HUWA NAMALIZA  SHIDA ZAKO 
cc to naxylady upo kwenye cue usitafute maarufu maana umaarufu hauji kwa njia za panya from Unstoppable
MA International Relations & Diplomacy