Thursday, 22 March 2018

MSICHANA ALIYEWAPIGA MAKOFI WANAJESHI AFUNGWA JELA…

Msichana wa Palestina Ahed Tamimi aliyerekodiwa kwenye kipande cha video akizozana na baadaye kuwapiga makofi wanajeshi wa Israel wenye bunduki, amehukumiwa kifungo cha miezi nane jela baada ya kukiri makosa.
Mwanasheria wake ameviambia vyombo vya habari kuwa, Tamimi amehukumiwa kifungo hicho sambamba na kulipa faini ya $1,440.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 ambaye video yake inayoonesha tukio hilo, ilizua gumzo mitandaoni alifanya kitendo hicho Disemba mwaka jana alipokuwa miongoni mwa wanaopinga hatua ya Marekani kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Tamimi alirekodiwa na mama yake mzazi karibu na eneo la nyumbani kwao, na wakati huo alikuwa na umri wa miaka 16.
Msichana huyo anaonekana kumpiga teke mwanajeshi mmoja na kumuongeza kofi huku akitishia kumpiga ngumi mwanajeshi mwingine.

Kundi la waandamanaji limeibuka katika eneo la Nabi Saleh wakipinga adhabu hiyo.Tayari watu milioni 1.7 wamesaini mtandaoni hati ya kutaka Tamimi aachiwe huru.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment