Sunday 4 March 2018

WATU WAPIGA KURA UCHAGUZI MKUU ITALIA…

Watu nchini Italia wanapiga kura baada ya kampeni zilizoangazia zaidi masuala la uhamiaji na uchumi.

Waandishi wa habari wanasema kuwa ni vigumu kusema ni nani atashinda katika kura hiyo.
Upande wa Five Star Movement, chama kinachotawaka, na mrengo wa kulia wa waziri mkuu wa zamani Silvio Berlusconi wote wametabiri ushindi.
Bw Berlusconi, 81, hawezi mweyewe kushika wadhifa wowote hadi mwaka ujao kutokana na kesi inayohusu kodi.

Kura za maoni zilipigwa marufuku wiki mbili zilizopita lakini uatafiti kabla ulionyesha kuwa muungano huo wa Berlusconi ulikuwa na nafasi ya kupata ushindi.

0 comments:

Post a Comment