Mwanamke
mmoja katika kijiji cha Nyahera Kaunti ya Kisumu nchini Kenya, amewaua watoto
watatu wa mke mwenzie, na kisha mwenyewe kujinyonga.
Tukio
hilo limeelezwa kwamba mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Jacinta Otieno,
aliwaita watoto hao wanne kwenda kunywa uji nyumbani kwake, na ndipo alipoanza
kuwacharanga na mapanga mpaka kuwaua na kisha mwenyewe kujinyonga, huku mtoto mmoja
akinusurika baada ya kukataa kwenda kunywa uji.
Jacinta
alifanya tukio hilo baada ya mke mwenzie kwenda kanisani na kuwaacha watoto
peke yao nyumbani, ambako wanaishi jirani, huku mume wao akiishi jijini Nairobi
na watoto wake wengine.
Kwa
mujibu wa majirani, wawili hao wameelezwa kuwa hawakuwa na maelewano mazuri
kutokana na wivu kwa mume wao, na kwamba Jacinta alishajaribu kutaka kujiua
wiki moja iliyopita.
Watoto
hao waliouawa walikuwa na umri wa miaka 7, 4 na 2, walikuwa wa mke mwenzie
Hellen Otieno.
0 comments:
Post a Comment