Jeshi
la Polisi Zanzibar limesema halina taarifa za kuonekana kwa mashekhe watatu wa
Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, ambao waliripotiwa kutoonekana tangu Januari 9,
mwaka huu.
Hayo
yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir Ali,
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa jeshi hilo
lilifanya kazi ya kuwatafuta mashekhe hao, lakini halikufanikiwa kuwaona.
Aidha
Kamanda huyo ameiasa jamii kuacha kuchanganya mambo ya kihalifu na kisiasa,
kwa kuwa halileti taswira nzuri kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Hata
hivyo Kamanda Ali ameongeza kuwa awali jeshi hilo lilipokea taarifa rasmi
kutoka kwa familia na ndugu wa mashekhe hao, kuwa hawaonekani na wamepotea
katika mazingira ya kutatanisha huku likihusishwa jeshi hilo kuwa ndio lililo
wachukua.
0 comments:
Post a Comment