Thursday, 22 March 2018

AMUUA MAMA YAKE KISHA KUMTOA MACHO….

Camille Balla 32, kutoka Florida amekamatwa baada ya kumuua mama yake Francisca Monterio-Balla na kisha kumtoa macho na kisha kupiga simu polisi na kuwaeleza kuwa yeye ni muuaji.

Hii ilitokea baada ya binti huyo kutumia madawa ya kulevya yaliompelekea kutokujielewa.
Baada ya polisi kufika eneo la tukio walikuta mwanamke huyo amekaa huku damu zikiwa zimetapakaa.Aliamka na kukimbia ndani ya nyumba na kisha kudai kuwa  yeye ni muuaji.
Mwanamke huyo alikamatwa na kudai kuwa alikuwa amevuta bangi kabla ya kumvamia mama yake na kisha kumuua.Jumatatu alikutanishwa na hakimu jumatatu lakini alinyimwa dhamana kutokana na kile alichokifanya.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment