Friday 16 March 2018

MUGABE: SIKUTEGEMEA KUONDOLEWA MADARAKANI NA MNANGAGWA

 

Aliyekua Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amevunja ukimya kwa mara ya kwanza tangu aondolewe Madarakani,kwa kusema kuwa amekua muhanga wa mapinduzi ya kijeshi.Akiongea na televisheni ya SABC ya Afrika kusini, Mugabe amesema Rais wa sasa Emerson Mnangagwa asingeweza kuingia madarakani bila kutumika kwa jeshi.Akiwa katika nyumba yake ya kifahari mjini Harare, Mugabe amekemea mbinu zilizotumika kumuondoa madarakani..Amesema alikua tayari kufanya mazungumzo na Rais wa sasa Emerson mnangagwa na angehakikisha mabadiliko ya madaraka ya uhalali na si yale ya kulazimishwa.Mugabe amesema kuwa Yuko tayari kwa ajili ya Mazugumzo na Mnangagwa ili kulinda katiba yao.Hakuna uhakika kama rais huyo wa zamani mwenye Umri wa miaka 94 Anataka kurudi madarakani ama la, lakini ni wazi kuwa anadhani amesalitiwa na rais wa sasa Emerson Mnangagwa.

0 comments:

Post a Comment