Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo nchini Tanzania imemshutumu
nwanamuziki maarufu Diamond Platnumz kwa kauli aliyoitoa kuhusu kufungiwa kwa
nyimbo zake mbili.
Waziri Dkt Harrison Mwakyembe
amesema "amesikitishwa" na kauli alizozitoa mwanamuziki huyo
akihojiwa na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo amesema maamuzi ya
kuzifingia baadhi ya nyimbo na wasanii wawili kwa kukiuka maadili yalifanywa
kwa mujibu wa sheria na siyo kwa utashi wa Naibu Waziri Juliana Shonza.
Mwanamuziki huyo wa kizazi kipya,
ambaye jina lake halisi ni Nassib Abdul, anadaiwa kumlaumu naibu huyo wa
waziri.
"Diamond atambue kuwa serikali
ina taratibu zake na maamuzi ya naibu waziri ni maamuzi ya wizara," Dkt
Mwakyembe amenukuliwa kwenye taarifa iliyotumwa na wizara hiyo kwa vyombo vya
habari.
Nyimbo
za Diamond zilizofungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA)
mwishoni mwa mwezi uliopita ni Hallelujah (uliomshirikisha
Morgan Heritage ) na Waka Waka (uliomshirikisha
Rick Ross).
Waziri huyo alisema kuna vikao vingi
vya wasanii ambavyo vimekuwa vikifanywa kati ya serikali na wasanii
"lakini Diamond hakuwahi kuhudhuria vikao hivyo."
"Si wajibu wa serikali
kumfanyia kikao cha peke yake."
"Sheria ni ya watu wote bila
kujali umaarufu au nafasi ya mtu katika jamii, hivyo msanii Diamond anapaswa
kutii sheria na mamlaka zilizowekwa."
Waziri huyo alimwambia mwanamuziki
huyo kwamba si busara kwake kushindana na serikali na kwamba endapo ana ushauri
wowote, ni vyema kwake kuuwasilisha kwa njia sahihi "lakini si kwa
kumshambulia waziri kwa dharau na kejeli kama alivyofanya."
Dkt Mwakyembe alisema Diamond
anatarajiwa kuwa mfano bora kwa wanamuziki wenzake kutokana na mafanikio
aliyoyapatta katika fani ya muziki.
"Napenda kuwakumbusha wasanii
wote kwamba sanaa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine, hivyo pamoja na kuwa na
kipaji hicho, wasanii wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo
inayosimamia tasnia ya sanaa kama ilivyo kwa tasnia nyingine," alisema Dkt
Mwakyembe.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na Chama cha Wasanii wa Muziki wa
Bongo Fleva (Tuma) na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, pia
walishutumu hatua ya mwanamuziki huyo ya kumshambulia naibu waziri huyo.
TCRA nayo ilisema kuwa inafuatilia
mahojiano yake katika kituo hicho kazi ambayo inafanywa na kamati yake ya
maudhui, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.
Afisa Mkuu Idara ya Utangazaji TCRA,
Andrew Kisaka alisema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika
katika kituo wanachokisimamia.
Kwa mujibu wa gazeti hilo la
Mwananchi, Bw Kisaka alisema mamlaka hiyo inanaangalia zaidi chombo ambacho
imekipa leseni na kwamba, masuala mengine yatashughulikiwa na mamlaka nyingine.
Basata kupitia katibu mtendaji wake,
Godfrey Mngereza walimtaka Diamond kufuata taratibu katika kulalamikia suala
hilo ikiwamo kuandika barua kama alivyoelezwa.
Alisema si lazima msanii aandikiwe
barua pale anapokosea kama ambavyo Diamond alitaka kupitia ukurasa wake wa
Twitter katika ujumbe aliouandika Jumanne.
Diamond aliandika: " Swala la Barua Unalijua leo baada ya Kukosa Point sahihi?
Ungekuwa unajua kama taratibu sahihi ni Kuandika Barua, Mbona hukuwatumia pia
Wasanii barua zakuwa unafungia kazi zao?... kwakuwa Uliyapeleka Social Media na
Radio, nami nikakupelekea huko ili uenjoy Zaidi...
0 comments:
Post a Comment