Tuesday 6 March 2018

AOMBA KUPELEKWA KWA MGANGA BADALA YA JELA…….

Mwanaume mmoja kwa jina la Wilson Obeka anaekabiliwa na mashtaka ya jinai, aliwashangaza wengi mahakamani huko Eldoret baada ya kumuomba hakimu apelekwe kumuona mchungaji au mganga badala ya kwenda jela.

Bwana huyo anakabiliwa na kesi ya kutishia kuua, kuvuruga amani pamoja na kujaribu kufukua maiti bila kufuata sheria.
Siku kesi yake inasikilizwa ili kujulikana kama yuko tayari kuendelea na kusikilizwa kwa kesi hiyo, alimwambia hakimu kuwa nimeona niko kwenye kesi nyingi na imefikia hatua sikumbuki aliyenishitaki.
Hivyo akaomba kupelekwa maombi au kwa mganga maana anahisi ameingiliwa na pepo bila kujijua.

Hakimu aliamuru bwana huyo apelekwe kuchekiwa akili kisha kesi yake itasikilizwa tena baadae..

0 comments:

Post a Comment